Na Mwandishi Wetu,Dodoma
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Magharibi Dkt.Johannes Lukumay,amesema jimbo hilo linachangamoto ya uhaba wa viwanja vya michezo licha ya kuwa na fursa kubwa ya michezo.
Dkt Lukumay ameeleza changamoto hiyo Mei 4,2026 Bungeni jijini Dodoma wakati akizungumza na Waziri Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Paul Makonda ambapo amesema kwa sasa serikali inatakiwa kuona umuhimu wa kuwekeza na kujenga Kiwanja cha kisasa katika jimbo hilo ili kuruhusu hata fursa nyingine kufunguka.
“Endapo kutakuwa na kiwanja bora cha michezo basi fursa mbalimbali zitaibuka,”amesema
Pamoja na hayo Dkt.Lukumay nyota wa soka la kimataifa kutoka Ivory Cost , Didier Drogba kuona fursa ya kwenda kuwekeza Academy ya kisasa katika jimbo hilo.
Akijibu ombi hilo Waziri Makonda amesema amelichukua na analifanyiakazi huku akisema Serikali ya awamu ya sasa imedhamiria kuhakikisha kuwa inaboresha lakini pia kujenga viwanja vingi vya michezo.

More Stories
Yas, yaendesha kambi huduma za macho bure Kilwa
Askofu Siso ampongeza Mzalendo Alphonce kwa kujitoa kwa jamii
Wananchi kata ya Mkinga wapongezwa kwa kuanzisha ujenzi wa Kituo Cha afya