Na Allan Ntana, Sikonge
JENGO la ofisi ya wataalamu lililokuwa likitumika kuhifadhi dawa, chanjo na vifaa tiba ikiwemo vifaa vya kufulia nguo za wagonjwa katika Kituo cha Afya Mazinge wilayani Sikonge mkoani Tabora limeteketea kwa moto pamoja na vifaa vyote vilivyokuwa vimehifadhiwa ndani.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri akiwa ameambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ametembelea jengo hilo na kujionea jinsi lilivyoteketea kwa moto.
Kufuatia tukio hilo ameunda kamati maalumu kwa ajili ya kufanya uchunguzi na kutakiwa kutoa taarifa ndani ya siku siku.
Amesema kuwa tukio hilo limeshtua wananchi wengi hasa kutokana na unyeti wa jengo lililoungua na uhalibifu mkubwa uliotokea. Amesisitiza kuwa kwa sasa hawawezi kuzungumza chochote kuhusiana na chanzo cha moto huo na hasara iliyopatikana.
Aliitaka kamati ya uchunguzi iliyoundwa kufanya kazi yake kwa weledi mkubwa na kutoa taarifa ndani ya muda huo huku akiahidi kuwa yeyote atakayebainika kuhusika atachukuliwa hatua za kisheria.
More Stories
Wataalamu wabobezi katika sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi wakutana nchini
Wizara ya afya yachukua hatua sakata la Mzazi anayedai kubadilishiwa Mtoto Arusha
EWURA yatangaza bei za Mafuta kwa mwezi Aprili 2025