Na Mwandishi Wetu ,Timesmajiraonline
BOHARI ya Dawa (MSD) imesema upatikanaji wa dawa na vifaa tiba nchini uko imara, ikiwa na akiba ya kutosha kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita, licha ya kuendelea kwa mzozo Mashariki ya Kati.
Ufafanuzi huo umetolewa leo na mwishoni mwa wiki na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai, alipokuwa akizungumzia na wahariri wa vyombo vya habari mkoani Dodoma katika kikao kazi kilichoandaliwa na MSD..
Amesema MSD imejipanga vyema kuhakikisha upatikanaji endelevu wa bidhaa hizo muhimu, huku ikieleza kuwa tayari kuna tathmini inayoendelea kufanywa na timu maalumu ya wataalamu ili kubaini hatari zinazoweza kujitokeza na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana nazo.
Amesisitiza kuwa juhudi zinaendelea kuimarishwa, hasa katika kuhakikisha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba vinavyoagizwa kutoka nje ya nchi hauathiriki na mabadiliko ya hali ya usalama na uchumi wa kimataifa.
Alisema Serikali itaendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa hali hiyo ili kuhakikisha huduma za afya nchini haziathiriki na wananchi waendelee kupata huduma bora bila usumbufu.
Katika hatua nyingine Mganga Mfawindhi wa Hospitali ya Dodoma Dkt. Joshua Mwalongo, ameishukuru MSD kubwa wanayofanya , kwani hata pale wanapoomba dawa kwa dharula wanapelekewa haraka.
Ameitoa pongezi hizo mwishoni mwa wiki Jijini Dodoma wakati alipozungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari walipotembelea hospitali hiyo kuona huduma zinazotolewa kupitia vifaa tiba na dawa kutoka MSD.
Amesema Sh.Bilioni 2.7 zimetumika hadi sasa katika ujenzi wa Hospitali ya Jiji la Dodoma, huku MSD ikiipatia vifaa tiba vya zaidi ya Milioni 100/.
Hospitali hiyo ambayo hadi sasa ina majengo 10 ya kutolea huduma , imeanza kutoa huduma Januari mwaka 2025 ambapo kwa sasa inatoa huduma kwa wagonjwa 700 kwa mwezi.

Dtk. Mwalongo ameishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa Hospitali hiyo ambayo imepunguza msongamano katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na Hospitali ya Makole ambapo wanamchi watapata huduma bora na kisasa karibu na maeneo yao, huku vifaa tiba vinavyotolewa na MSD vikiwa vya kisasa.
Awali Meneja MSD Kanda ya Dodoma, Mwanashehe Jumaa amesema kupatika kwa Hospitali ya Jiji sambamba na vifaa tiba vinavyosambazwa MSD itasaidia kutoka huduma za uhakika na kupunguza msomgamano katika Hospitali zingine .
Amewahakikishia Watanzania kuwa. MSD itaendelea kupeleka Dawa na vifaa tiba vya kisasa kwa wakati.

Katika hatua nyingine MSD imeelezwa hatua mbalimbali za mafanikio ambazo zimefikiwa ba bohari hiyo katika kipindi cha miaka minne.
Mfamasia kutoka kitengo cha Mipango,Ufuatiliaji na Tathimini wa MSD,Lilian Bwiro, amesema kumekuwepo na mafanikio katika kipindi cha miaka minne 2021/22 hadi mwaka 2024/25.
Amefafanua katika kipindi cha miaka minne mapato ya MSD yameongezeka kwa asilimia 103 kutoka Sh.Bilioni 315.12 hadi kufikia kiasi cha Sh.Bilioni 640,5 mwaka 2024/25.
Pia mafanikio mengine ni kuongezeka kwa upatikanaji wa bidhaa za afya ashiri kutoka asilimia 42 mwaka 2021/22 hadi kufika asilimia 73 Machi, 2026.
“Hali ya utimizaji wa mahitaji wa vituo vya kutolea huduma za afya umeendelea kuongezeka kutoka asilimia 4l hadi kufikia asilimia 77 katika kipindi cha miaka minne.”
Pia amesema mafanikio mengine ni kuongezeka kwa mizunguko ya usambazaji wa bidhaa za afya kwenda vituo vya kutolea huduma za afya kutoka mizunguko minne kwenda mizunguko sita kwa mwaka ,huku ununuzi wa bidhaa za kuwezesha uzazi pingamizi ( CEmONO) ukifikia asilimia 100 ya MS.
Magesa ameongeza kuwa mafanikio mengine mashine 162 za kusafisha damu(dialysis) zimesambazwa kutoka mashine 60 mwaka 2021/2022 zilizogharimu Sh.bilioni 10.14
Pia kukamilisha ujenzi wa maghala ya kisasa yanayokidhi viwango vya uhifadhi na kuanza kutumika katika Kanda ya Dodoma na Mtwara -mita za mraba 12,000.
Aidha kuanza kwa ujenzi wa ghala la Chato mkoani Geita lilifikia asilimia 42 ya utekelezaji.
Mafanikio mengine ni uanzishwaji wa kampuni tanzu ijulikanayo kama MSD Medipharm Manufacturing Company yenye jukumu la kusimamia uzalishaji unaotekelezwa kibiqshara na kwa ufanisi mkubwa .
“Pia kiwanda cha mipira ya mikono -Idofi kukamilika na kuanza kazi rasmi ya uzalishaji Februari 2024 pamoja na ongezeko la thamani ya bidhaa zinazonunuliwa kutoka kwa wazalishaji wa ndani kutoka Sh.bilioni 15.90 zilizonunuliwa mwaka 2021/22 hadi Sh.bilioni 98.72 mwaka 20/2024/25.”

More Stories
Kibong’oto yapiga hatua mapambano dhidi ya TB
Wanawake Watwishwa zigo la kusimamia maadili katika jamii
WATU WASIOJULIKANA