Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Ubalozi wa Italia nchini Tanzania, kwa kushirikiana na Wakala wa Biashara wa Italia na Karimjee Group,imetangaza rasmi maonesho yenye jina la “Glass Bridge – Murano Meets Shanga”, yanatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Rangi Gallery kuanzia Machi 28 hadi Aprili 4,2026.
Maonesho hayo yanaandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Italia pamoja na Wizara ya Utamaduni ya Italia ili kuonesha ubunifu na usanifu wa Italia duniani kote.
Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam kwa vyombo vya habari, ilisema kwa mwaka huu Kaulimbiu ya toleo la 10 la mwaka huu ni “RE-DESIGN Regenerating spaces, objects, ideas, relations”.
Imesema maonesho hayo yatakayofanyika katika ukumbi wa Rangi Gallery ambapo yanatarajia kuanza na mazungumzo ya kipekee kati ya ubora wa ubunifu wa Italia na ustadi wa ufundi wa Tanzania vitakavyooneshwa ni pamoja na mkusanyiko maalum wa taa za kisasa kutoka Foscarini, pamoja na vyungu vya kioo vya Murano vilivyotengenezwa kwa mikono na kazi za sanaa za Murano-Shanga.

Imesema foscarini ni chapa ya ubunifu wa Italia iliyoanzishwa mwaka 1981 katika kisiwa cha Murano, karibu na Venice.” kampunl hii hutengeneza taa za juu zinazochanganya ufundi wa jadi hasa kioo cha Murano na teknolojia ya kisasa pamoja na vifaa vya ubunifu. Utamaduni wa utengenezaji wa kioo katika eneo la Venice ulianza takriban karne ya 8 na kuhamia katika kisiwa cha Murano katika miaka ya 1200.
“Murano pla inajulikana kwa vyungu vyake vya kioo (vinavyojulikana kama Murano], ambavyo hutengenezwa kwa mikono na mafundi stadi wanaoyeyusha na kuunda kioo katika joto la juu, na kuunda vipande vya kipekee mara nyingi vilivyopambwa kwa rangi ang’avu, dhahabu na michoro tata. Vikijulikana kwa ubora wa hali ya juu na thamani ya kisanil, kila chungu huwakilisha mchanganyiko wa ufundi wa karne nyingi na urithi wa kitamaduni wa Italia,”imesisitiza sehemu ya taarifa hiyo

Aidha imesema maonesho haya pia yatahusisha kazi za Shanga (Kutoka Arusha], taasisi ya kijamii ya Tanzania Inayovutia na iliyowaajiri watu wenye ulemavu kuzalisha vito vya mapambo, bidhaa za kioo na mapambo ya nyumbani kwa kutumia vifaa vilivyorejelewa. Kupitia mradi wa “Glass Bridge”uioanzishwa mwaka 2025 kwa juhudi za mbunifu Emmanuel Babled na kampuni yake ya Tanzania ya Kukua, mafundi wakuu wa Murano (mastri vetrai) wameshiriki utaalamu wao na wasanil wa Shanga, kuwezesha utengenezaji wa vyungu vya kioo kwa mtindo wa Murano na kubadilisha taka kuwa sanaa,kwa kuunganisha kwa uzuri utamaduni wa Italia na ubunifu wa Tanzania, mradi wa “Glass Bridge” pla unakuza uchumi, mzunguko na uendelevu.
Taarifa hiyo ilisema kwa kuleta pamoja taasisi hizo tatu Foscarini, Murano na Shanga maonesho haya yanaonesha jinsi ubunifu unavyoweza kuwa daraja kati ya tamaduni, ukiunganisha ubora wa kimaumbo, ubunifu na athari za kijamii.

More Stories
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini
REA imeleta mageuzi sekta ya nishati