
Na Israel Mwaisaka, Rukwa
Afisa elimu msingi wilayani Nkasi Eliud Njogela amepongeza jitihada za Wananchi wa Kijiji Cha Korongwe kwa juhudi walizozianza za kujenga vyumba 4 vya madarasa kwa njia ya kujitolea ili kupunguza msongamano wa Wanafunzi madarasani katika shule hiyo.
Amesema kuwa shule hiyo Ina idadi kubwa ya Wanafunzi ikilinganishwa na vyumba vilivyopo vya madarasa kwani Ina Wanafunzi 3150 na madarasa yaliyopo ni 15 na yanayohotajika ni madarasa 70 yanayohitajika ni 55 na kuwa kitendo Cha Wananchi kujitolea kuanza kujenga vyumba vipya vya madarasa katika shule shikizi ya forodhani ni mikakati muhimu wa kukabiliana na changamoto hiyo.

Amesema Serikali inao mpango wa kusaidia nguvu za Wananchi kwa kuezeka vyumba hivyo vya madarasa kwani mpaka Sasa madarasa hayo yamewekwa kwenye mpango wa bajeti hivyo bajeti hiyo itakapoanza kutekelezwa na vyumba hivyo vya madarasa navyo vitaezekwa.
Alidai kuwa lengo la Serikali ni kutaka kuifanya shule hiyo shikizi kuwa shule kamili ikiwa ni pamoja na kuongeza shule nyingine ya tatu na kuwa hilo ndilo litakua suluhisho la changamoto ya idadi kubwa ya Wanafunzi katika shule hiyo.
Awali Mwenyekiti wa Kijiji Cha Korongwe Forodhani Konrad Sokoni alidai kuwa changamoto ya uwingi wa Watoto katika shule hiyo ndicho kilichowasukuma wao kujitoa na kuanza kujenga vyumba vya madarasa kwa njia ya kujitolea ambapo walianza na msingi wa vyumba sita lakini hadi Sasa ni vyumba 4 vimefikia kiwango Cha rinta na kuiomba Serikali isaidie kwa kuezeka madarasa hayo.
Amesema kuwa Kuna jitihada mbalimbali ambazo wao kama kijiji wamekua wakizifanya za kupunguza changamoto hiyo lakini walikubaliana kuchangishana na Kutoa nguvu zao na kufanikisha kuanzisha misingi ya vyumba 6 vya madarasa na Vinne kufikia kiwango Cha rinta na kuwa kwa Sasa wanauhitaji msaada wa Serikali kwa kuezeka madarasa hayo.

Diwani wa kata ya Korongwe Hamisi Mtaho kwa upande wake ameiomba Serikali kuthamini nguvu za Wananchi kwa kuezeka majengo hayo ambayo ni nguvu ya Wananchi na kuwa hilo litawatia nguvu Wananchi ya kuendelea kujitolea.
Amesema kuwa licha ya kuendelea kuwasilisha changamoto hiyo Serikali bado ataendelea kuwasiliana na Wadau mbalimbali wa maendeleo akiwemo Mbunge wa jimbo katika kuona wanakusanya nguvu za pamoja katika kuona kwamba lengo lao linatimia.


More Stories
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni
Mbega ataka viongozi kuimarisha ulinzi kudhibiti wageni.
Kero za Walimu kutoshughulikiwa kwa wakati chanzo Cha msongo wa mawazo-CWT