*Ukarabati uwanja wa ndege Sumbawanga wafikia asilimia 96
Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online-Rukwa
Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Mwakiposa Kihenzile, ametoa wito kwa sekta binafsi na kampuni za ndege kuwekeza katika huduma za usafiri wa anga.
Kihenzile ametoa wito huo Februari 21, 2026 akiwa mkoani Rukwa, ambapo amekagua hatua mbalimbali za maendeleo ya ukarabati wa uwanja wa ndege Sumbawanga.
.
Ameeleza kuwa wito huo unalenga kupunguza changamoto zilizopo na kufungua fursa zaidi za kiuchumi kwa wananchi na wawekezaji.
Naibu Waziri huyo ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha viwanja vya ndege ili kuimarisha miundombinu ya sekta hiyo
Akitoa taarifa ya maendeleo ya ukarabati wa uwanja huo,Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Rukwa ambaye ni msimamizi wa mradi huo, Mhandisi Joseph Jemonge,amesema, utekekalezaji wa mradi huo umefikia asilimia 96 huku kazi zilizobaki zikihusisha hatua za mwisho kabla ya kuanza kutumika rasmi.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo wa Uchukuzi,amesisitiza umuhimu wa kukamilika kwa wakati kwa kazi zilizobakia ili kiwanja kianze kutoa huduma.
Wananchi na viongozi wa Mkoa wa Rukwa wameeleza matumaini yao ya kuanza kutumika kwa kiwanja hicho hivi karibuni.
Mradi huo unatarajiwa kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za biashara mkoani Rukwa.

More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama