November 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bilionin 8.3 kukamilisha miradi 22 ya maji

Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza

JIJI la Mwanza limepokea takribani bilioni 8.3, kwa ajili ya kukamilisha miradi 22 ya maji vijijini katika Wilaya tano huku Mkuu wa Mkoa huo John Mongella akiwasisitiza watendaji wa Halmashauri na Wakala wa Maji Vijijini na Usafi wa Mazingira (RUWASA) kusimamia kikamilifu ili ikamilike kwa wakati.

Akizungumza wakati akipokea mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hiyo Mongella amesema, miradi hiyo itakapokamilika inatarajia kuhudumia wakazi takribani 120,000.

Amesema, miradi hiyo 22 ina urefu wa takribani kilometa 238 huku pia wakipokea karibu milioni 900 kwa ajili ya kujenga uwezo wa vyombo vya usimamizi wa maji.

Amesema, katika awamu hiyo ya kwanza wamekupokea mabomba ambayo yanaenda kufanya kazi kwenye maeneo 22 ya miradi hiyo ambapo Meneja wa RUWASA Mkoa amesema wanategemea hadi kufikia mwaka mpya 2021, miradi hiyo itakuwa imekamilika na kuanza kutoa maji safi na salama kwa wananchi wote.

“Namshukuru Rais Magufuli hii miradi aliiasisi mwenyewe na sasa tunaona utekelezaji wa kasi wa ahadi zake na huu ni mpango unaoendelea na utekelezaji unaendelea, wasije kufiriki ni kwasababu tupo kwenye kipindi cha uchaguzi kwani sasa Serikali haisimami kuhakikisha wananchi wanapata huduma na hii siyo mpango mpya ni mpango endelevu ya kuhakikisha wananchi wetu wanapata maji safi na salama,” amesema Mongella.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akizungumza baada ya kupokea mabomba kwa ajili ya utekelezaji wa miradi 22 ya maji vijijini katika Wilaya tano Mkoani Mwanza. (Picha na Judith Ferdinand)

Hata hivyo alitoa rai kwa mamlaka za Halmashauri na RUWASA Mkoa kuwa vifaa vimeishafika hivyo wahakikishe wanasimamia miradi hiyo ikamilike kwa wakati na ikiwezekana ikamilike kabla ya muda ili wananchi wapate maji mapema.

Meneja RUWASA Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Immaculata Emmanuel amesema, wanatekeleza miradi hiyo 22 kwenye Wilaya za tano sawa na Halmashauri sita ikiwemo ya Magu, Kwimba, Sengerema na Buchosa, Misungwi na Kwimba pamoja na Ukerewe huku Wilaya za Ilemela na Nyamagana hazipo kwenye mpango huo kwa vile zinasimama na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA).

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Mwanza Mhandisi Immaculata Emmanuel, akizungumza wakati wa upokeaji mabomba ambayo yanaenda kutumika kwenye utekelezaji wa miradi 22 ya maji vijijini katika Wilaya tano Mkoani Mwanza.

Amesema, miradi ya aina hiyo imetekelezwa katika Mikoa 17 kati ya 25 Tanzania Bara ikiwemo Mkoa wa Mwanza wenye miradi 22 vijijini ambayo itawanufaisha wananchi zaidi ya 100,000 ambapo kati ya fedha bilioni 7.15 zinatumiwa kwa ajili ya miundombinu,hivyo alihadi kufikia Desemba mwishoni watakuwa wamekamilisha miradi hiyo.

Mhandisi wa Maji RUWASA, Exaud Humbo amesema, wananchi watarajie kupata maji kwa kipindi kifupi kwani kazi inaendelea na katika miradi hiyo 22 imegawanyika ambapo Magu mitano, Misungwi miwili, kwimba mitano,Ukerewe minne Sengerema na Buchosa sita,