Na Judith Ferdinand, Mwanza
MGOMBEA ubunge Jimbo la Ilemela kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM)Dkt. Angeline Mabula amewaahidi wakazi wa Kata ya Shibula na Pasiansi neema katika masuala mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu,afya, barabara na maji.
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata hizo mbili katika mikutano yake ya kampeni iliofanyika uwanja wa Shibula Centre Kata ya Shibula na Bwiru Msikiti Kata ya Pasiansi,ambapo amewaomba wananchi kuchagua mafiga matatu yaani rais,mbunge na diwani anayetokana na CCM ili kwa pamoja waweze kutekeleza ahadi hizo.
Dkt.Angeline,amesema katika Kata ya Shibula anatambua kuwa ina shule moja tu ya sekondari inayoitwa Shibula hivyo itajengwa ya pili na pia anatambua ana tambua hakuna shule ya msingi nayo itajengwa kwa ushirikiano wa utatu.
“Shibula ni kubwa ina mitaa 14,lakini inashule ya sekondari moja tu,watoto wanatembea umbali mrefu tutafanya kila linalowezeka tupate sekondari ya pili na kama hiyo haitoshi Shibula yenyewe haina shule ya msingi watoto wanakwenda mbali kwaio hapa tunalo jukumu Swila Dede( mgombea Udiwani) na wananchi wako na ofisi ya Mbunge na Mkurungezi kuhakikisha tunapata shule mpya ya sekondari na msingi Shibula,” amesema Dkt.Angeline.
Dkt.Angeline amesema zimetengwa milioni 95 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa vitatu shule ya msingi Igogwe na kimoja shule ya sekondari Shibula pamoja na matundu ya vyoo 10 katika shule hiyo kwani anatambua bila ya kuwa na vyoo vya kimkakati vinavyojali na watu wenyewe ulemavu mambo hayawezi kuwa sawa.
Huku milioni 45 zimetengwa kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu Kata ya Pasiansi ambazo zitaboresha vyumba vya madarasa shule ya msingi Mnarani na kujenga nyumba ya walimu, watapeleka madawati 100 shule ya msingi Bwiru, kuwa na matundu ya vyoo 10 shule ya Sekondari Kitangiri.
Dkt.Angeline amesema,ilani ya uchaguzi ya CCM inazungumzia barabara ya Airport,inayopita Sangabuye, Bugogwa, Shibula, Kayenze na kuelekea Nyanguge ina urefu wa kilomita 46 ambapo upembuzi yakinifu unafanyika na itawekewa lami, pia wametengewa milioni 612 kwajili ya kutengeneza barabara za Bukala-Ilalila,Igogwe kwenda Kabusungu mpaka Sangabuye Sekondari na Kahama- Igombe kupitia Ililali ambayo inaenda kutengeneza kwa kiwango cha changarawe.
Huku zaidi ya milioni 155 zimetengwa kwa ajili ya kutengeneza na kurekebisha barabara za Kata ya Pasiansi na maeneo korofi ikiwemo inayo unga kwenda Jiwe Kuu pia watataka watu wenyewe daladala waanze kupita Bwiru-Breweries na kutokezea Iloganzala kwa ajili ya kurahisisha usafiri pia wana ujenzi wa daraja la mchangani zimetengewa fedha na barabara inayoenda ziwani tayari imeomvewa fedha kwa andiko maalum.
Pia amesema,sekta ya afya ilikuwa na changamoto nyingi ikiwemo kutokuwa na miundombinu ya kutosha na majengo ya mama na mtoto tangu wameingia 2015 wamefanya kazi kubwa ya kuhakikisha vinaboreshwa ikiwemo kituo cha afya Karume ambacho kipo jirani na wanashibula na awali wote walikua Kata moja,pia kituo cha Afya Buzuruga ambacho kimeboreshwa na kinaanza kutoa huduma ya upasuaji wiki ijayo.
Aidha amesema,eneo la zahanati ya Pasiansi linatosha kuwa kituo cha afya cha Kata hiyo kinachisubiliwa sasa ni kulipwa fidia kwa kaya zilizopo pale ambazo hazizidi tano.
“Unapo boresha sekta ya afya unapunguza vifo vya mama na mtoto mara nyingi mama anapokuwa mjamzito kifo kwake uwa ni cha karibu sana kama hakuna huduma,lakini sasa hivi toka Dkt John Magufuli ameingia madarakani jimbo letu la Ilemela vifo vya kina mama vilivyokuwa vinatokea ni 20 kati ya wanawake 1000 kwa mwaka 2015 waliokuwa mwaka 2020 vifo ni vitatu tu, watoto 45 waliokuwa wanapoteza maisha 2015 sasa hivi ni watoto 7 kati ya watoto 1000,ambapo hayo yote ni mafanikio makubwa katika sekta ya afya,” amesema Dkt.Angeline.
Aidha amesema,kulikua na watumishi 212 sekta ya afya lakini sasa wapo 400, na zaidi ya 47 wamepandishwa madaraja na wametoa wabobezi(specialist) wawili huku akiahidi kuwa wataenda kufanya kazi ya kuhakikisha maji yanaongezeka kwani kuna chanzo cha maji Kabangaja na Butimba hivyo waendelea kuwaamini wanaenda kupata maji kwani awali maji yaliokuwa yamepangwa kata ya Kahama ni ya visima vinane wakati wanaitwa vijiji sasa ni mitaa hivyo miundombinu iliopo ilikuwa imetengenezwa kama ya vijiji.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea