May 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

920 waanza mtihani wa kidato cha sita Ilemela

Judith Ferdinand,TimesMajira Online,Mwanza

Jumla ya watahiniwa 920 wa kidato cha sita kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela,leo Mei 2,2023 wameungana na wanafunzi wengi nchini wa kidato hicho kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya sekondari.

Mtihani huo ambao umeanza leo Mei 2 utafanyika hadi Mei 22, mwaka huu,ambapo kwa Halmshauri hiyo kati ya watahiniwa hao wasichana ni 647 na wavulana ni 255.

Hayo yamebainishwa na  katika taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Violencea Mbakile.

Ameeleza kuwa kati ya watahiniwa hao,watahiniwa wa shule ni 846 ambapo wasichana ni 630 na wavulana ni 216.

Huku watahiniwa wa kujitegemea wakiwa 41 na kati yao wasichana ni 10 na wavulana 31 na kwa upande wa  watahiniwa wa ualimu ni 15 kati yao wasichana 7 na wavulana 8.

“Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ina jumla yavituo 10,vya kufanyia mtihani ambapo vituo 8 ni kwa sjili ya watahiniwa wa shule na viwili kwa ajili ya watahiniwa wa kujitegemea na ualimu,”.

Hata hivyo uongozi wa halmashauri hiyo umewahimiza watahiniwa hao kuhakikisha wanazingatia taratibu zote za mitihani huku ikiwatakia heri na baraka wanafunzi wote wa kidato cha sita katika kufanya vyema kwenye mitihani yao.