Na Na Tiganya Vicent, Tabora
MAKADA mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi katika majimbo ya Wilaya ya Tabora na Uyui wamezidi kuchukua na kurudisha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kwa tiketi chama hicho.
Kaimu Katibu wa Wilaya ya Tabora Violet Kassanga amesema jana jioni kwamba katika jimbo la Tabora Mjini wagombea 32 walikuwa wamechukua fomu, wanawake wakiwa watatu na wanaume 29.
Amesema kuwa hadi mchana Makada 10 akiwemo Mtaalamu wa Maabara kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(Uyui) Joseph Gibuya walikuwa wamerejesha fomu za kuomba kuteuliwa.
Kwa upande wa Katibu wa Wilaya ya Uyui, Neema Lunga amesema hadi kufikia jana jumla ya wanachama 25 wa Majimbo ya Tabora Kaskazini na Igalula walikuwa wamechukua fomu.
Amesema katika jimbo la Igalula wanachama sita wamejitokeza kuomba kuteuliwa na Tabora Kaskazini walikuwa wamejitokeza wanachama 19.
Miongoni mwa waliojitokeza kuomba kuteuliwa katika Jimbo la Tabora Kaskazini ni aliyekuwa Mbunge mwaka 2010 hadi 2015, Shaffir Sumar na Mbunge aliyemaliza muda wake Almas Maige.
Kwa upande wa Jimbo la Igalalu wanaomba ni pamoja na aliyewahi kuwa Mbunge wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne Injinia, Athuman Mfutakamba na Mbunge anayemaliza muda wake Mussa Ntimizi.
More Stories
TARURA Kilimanjaro yatimiza ahadi ya Rais Samia
DCEA,Vyombo vya Ulinzi na Usalama vyafanya operesheni ya kihistoria
Wananchi wakubali yaishe Bangi kubaki historia Tarime