January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Prof. Ndalichako, Mkenda wapeana wosia Dodoma

Na Joyce Kasiki, Timesmajira Online, Dodoma

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu ,Kazi,Ajira,Vijana na Wenye Ulemavu  Profesa Joyce Ndalichako na Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda wamekabidhiana ofisi huku kila mmoja akimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumuamini katika nafasi walizoteuliwa sasa.

Profesa Ndalichako ambaye alikuwa Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia sasa amepewa jukumu katika Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi Ajira na wenye Ulemavu huku   Profesa Mkenda akitokea Wizara ya Kilimo.

Akizungumza kabla  ya  makabidhiano hayo,Profesa Ndalichako amesema  wizara hiyo pamoja na mambo mengine ina miradi mingi inayoitekeleza na tayari imeshaanza na kwamba  fedha za utekelezaji wa miradi hiyo zipo.

 Amesema miongoni mwa miradi inayotekelezwa ni pamoja na uimarishaji wa Elimu msingi,sekondari,Elimu ya juu na  miradi ya kupambana na UVIKO 19 huku akisema miradi yote hiyo imelenga katika uoboresjai wa elimu nchini.

Profesa Ndalichako aliutumia nafasi hiyo kuwashukuru watumishi wote wa Wizara hiyo kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kipindi chote alichokuwa katika Wizara hiyo.

Amewasihi watumishi hao kuendeleza ushirikiano huo kwa Profesa Mkenda ili sekta ya Elimu nchini iendelee kusonga mbele.

Kwa upande wake Profesa Mkenda ambaye amehamishiwa Wizara hiyo kutoka wizara ya kilimo, aliwasihi watumishi wa wizara hiyo kutokuwa waoga katika kuzungumza kile wanachokijua mbele yake kwani bado anajifunza.

“Kwa Sasa Mimi bado mwanafunzi majifunza,sitaacha kukupigia Simu pale ninapohitaji ushirikiano wako (Profesa Ndalichako),lakini hata ninyi watumishi wenzangu,ninahitaji ushirikiano wenu,

“Kwa hiyo tunapokuwa kwenyeake vikao msiogope kuzungumza maana Mimi nategemea kujifunza mamboengi kutoka kwenu,kwa hiyo hata tunapokuwa vikaoni na mkaona siendi sawa sawa ,zungumzeni kwamba hapa siyo sahihi,na mkiona nimekomalia basi omba appointment tukutane ofisini ili unifahamishe zaidi.”amesema Profesa Mkenda na kuongeza kuwa 

“Nitatumia wiki tatu kupita kila idara kupata maelezo kuhusu shughuli zake,lengo kupata uelewa wa kutosha juu ya wizara hii na kuinua sekta ya Elimu kwa ujumla.”alisisitiza Profesa Mkenda

Aidha amempongeza Profesa Ndalichako kwa kuhudumu katika Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa muda mrefu na kwa mambo mengi mazuri aliyoyafanya katika Wizara hiyo.”amesema Profesa Mkenda