Na Mwandishi Maalum, Jeshi la Zimamoto
JESHI la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Morogoro limefanikiwa kuudhibiti moto uliowaka katika gari la mafuta lenye namba za usajili T862 BZS na tela namba T814 DBZ katika eneo la Kiegea, Wilayani Kilosa.
Gari hilo mali ya kampuni ya INTERPETROL lililokuwa limepakia shehena kubwa ya mafuta aina ya dizeli na lilikuwa njiani kuelekea nchini Burundi likitokea Jijini Dar es Salaam lililokuwa likie ndeshwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina la Hamidu Issa raia wa Burund.
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto (SACF), Goodluck Zelote amesema, walifanikiwa kuudhibiti moto huo na kuokoa kiasi kikubwa cha mafuta yaliyokuwemo.
Amesema, moto huo haukuleta madhara yoyote kwa binadamu na chanzo chake hakijafahamika mara moja japokuwa inasadikika kuwa ni hitilafu katika mfumo wa umeme wa gari hilo.
Hata hivyo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetoa rai kwa wananchi kutoa taarifa ya moto na majanga mengine kwa haraka zaidi kwa kupiga namba ya dharura 114.
Hivi karibuni kumekuwa na muendelezo wa matukio ya ajali za magari ya kubebea mafuta kuwaka moto na kulipuka yawapo barabarani yakisafirisha mafuta na kuleta madhara kwa binadamu, uharibifu wa miundombinu na mali zipakiwazo katika magari hayo.
More Stories
Mhandisi Samamba awasisitiza maafisa madini kusimamia usalama wa migoni msimu wa mvua
Wapinzani kutimkia CCM ishara ya ushindi Uchaguzi Serikali za Mitaa
Vikundi Ileje vyakabidhiwa mikopo ya asilimia 10, DC Mgomi avipa somo