October 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zidane afafanua kilichosababisha Bale asisafiri na Timu

Klabu ya Real Madrid itacheza na Mnachester City bila nyota wake makini Gareth Bale. Nyota huyo hakutajwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 watakaovaana na Manchester City mchezo wa ligi ya mabingwa utakaopigwa hii leo august 7.

Kocha wa Real Madrid amenukuliwa akisema ” Kuna uhusiano wa kinidhamu kati ya wachezaji na kocha ila jambo moja naloweza kusema ni kuwa Bale hataki kucheza mchezo  dhidi ya Manchester City.

Alipoulizwa kuhusu uwepo wa Bale ndani ya Real Madrid alisema Bale ni mchezaji wa Real Madrid na tunaheshimu hilo,mambo mengine yanafaa kujadiliwa kati ya mwalimu na mchezaji. Kwa sasa siwezi kuwaambia chochote,Ameamua kuto kucheza na sisi tunaangalia mchezo wetu wa leo.
Kikosi cha Real Madrid kipo jijini Manchester kwa ajili ya mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Etihad hii leo majira ya saa 4 kamili usiku