Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Simanjiro
Ziara maalumu ya Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Dkt. Suleiman Hassan Serera katika Bwawa la Irkishrot lililopo kwenye Kijiji cha Irkujit, Kata ya Endonyongijape.
Bwawa hilo muhimu linawekewa kingo ili kuzuia maji yasitoke, kuongezewa ukubwa sehemu maji yanapoingilia ili kuwezesha kina cha maji kuongezeka na hivyo kufanya maji mengi zaidi kutuama na kukaa kwa muda mrefu zaidi.
” Uboreshaji wa Bwawa hili utasaidia mifugo kuwa na uhakika zaidi wa kupata maji kwa kipindi kirefu, hususani kutumika wakati wa ukame” amesema Dkt. Serera.
Lengo ni kukagua kazi inayoendelea lakini kubwa ni kujua kama mkandarasi yuko kazini ama laa, ni bwawa la linalorekebishwa, ambalo limegharimu jumla ya sh.mil.144,321,198, ambapo awali liligharimu jumla ya sh.mil.127.
Aidha fedha hizo zimetolewa na Global Environment Fund ( GEF ) kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, mradi unajengwa na Mkandarasi SIMJO TECH.CO.LTD.”
Utekelezaji wa mradi huo ulianza Julai 7, 2022 na unatarajia kukamilika Desemba 21, 2022.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini