Na Jaala Makame Haji – ZEC
TUME ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC imetangaza wajumbe 18 kutoka Chama Cha Mapinduzi kwa nafasi ya Viti Maalum vya Wanawake vya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Tume imetangaza majina ya Wajumbe hao katika mkutano wake uliofanyika tarehe 07/11/2020 katika ukumbi wa mikutano wa Tume hiyo Maisara mjini Zanzibar.
Tangazo hilo limetolewa baada ya kuridhika kuwa wote wanasifa ya kuwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kama zilivyoainisha katika Katiba ya Zanzibar ibara ya 68.
Waliotangazwa na Tume ya Uchaguzi ni pamoja na Panya Ali Abdallah, Bihindi Hamad Hassan, Salma Mussa Bilali, Shadya Moh’d Suleiman, Fatma Ramadhan Mohamed (Mandoba), Sada Ramadhan Mwenda na Mwantatu Mbaraka Khamis.
Wengine ni Zainab Abdalla Salum, Riziki Pemba Juma, Leila Muhamed Mussa, Salha Mwinyi Juma, Hudhaima Mbarak Tahir, Sabiha Fil fil Thani, Aza Januar Joseph, Mwanaid Kassim Mussa, Mgeni Hassan Juma, Mwanajuma Kassim Makame na Rahma Kassim Ali.
Tume tayari imeshawasilisha Majina ya Wajumbe hao kwa Katibu wa Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya Hatua nyengine za Kisheria.
More Stories
Serikali ,Washirika wa Maendeleo waweka mkakati utekelezaji Dira ya 2050
Benki ya Exim yazindua suluhisho la malipo ya kisasa kwenye Z- Summit 2025
DCEA yateketeza zaidi ya ekari 300 za bangi