December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zari ampiga chini King Bae wake

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

MFANYABIASHAARA na Mzazi mwenza wa staa wa Bongofleva

na bosi wa Wasafi Media, Diamond Platnumz, Zarina

Hassan maarufu kama ‘Zari the boss lady’ameamua

kumpiga chini mpenzi wake maarufu kwa jina la King bae

2 au Dark Stallion, baada ya kuona hana manufaa naye.

Zari ambaye anaishi Afrika Kusini pamoja na watoto

wawili wa Mondi, aliandika ujumbe kwenye insta story

yake,kuwa mwanaume huyo inabidi amuache kwani hana

faida yoyote kwake.

“Nimemmisi, lakini inanibidi nimuache aondoke. Kwa

sababu kama hanijengi, hana faida kwangu siwezi

kuendelea naye,” ameandika Zari

Kufuatia hali hiyo baadhi ya mashabiki wamedai kuwa

hii inaweza kuwa muda muafaka kwa Mondi kurudisha

majeshi kwa Zari baada ya Dark Stallion ambaye alikuwa

raia wa Nigeria kutimuliwa.