June 5, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zao la Pareto Lawa Kipaumbele — Serikali Yajipanga Kurejesha Bodi Maalum

Zao la Pareto Lawa Kipaumbele — Serikali Yajipanga Kurejesha Bodi Maalum

‎ Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

‎MBUNGE wa Mbeya Vijijini  Oran Nnjeza ameeleza  changamoto kubwa katika mnyororo wa thamani wa zao la pareto licha ya Tanzania kuongoza Afrika kwa uzalishaji wa zao hilo.

‎Njeza ameeleza changamoto hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza Bungeni jijini Dodoma Leo Juni 3,2025.

‎“Mkulima huuza kwa shilingi 3,700 kwa kilo, mnunuzi akisaga huuza kwa 6,000, lakini crude extract huuza kwa 200,000 na ikishafikia kiwango cha refined ni hadi milioni moja kwa kilo. Mkakati uliopo hauwanufaishi wakulima wala nchi,” alisema Njeza.

‎Mbunge huyo alitoa hoja ya kurudishwa kwa bodi maalum ya kusimamia pareto ili kuongeza tija kwa wakulima na kusaidia nchi kupata viuatilifu vya asili (organic) kutoka ndani.

‎Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde alithibitisha kuwa Serikali inalipa kipaumbele zao hilo na kwamba hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa.


‎ “Tangu Mheshimiwa Rais aingie madarakani, mazao yaliyokuwa yamesahaulika sasa yameanza kuinuka, likiwemo zao hili la  pareto ambalo kwa sasa linasimamiwa na Bodi ya Mazao Mchanganyiko, lakini mipango ya kuliwekea bodi maalum ipo kulingana na ongezeko la uzalishaji,” alisema Silinde


‎Vle vile alisema,Serikali pia imeweka katika mipango kufufua kiwanda cha kuzalisha viuatilifu vinavyotokana na pareto ili kuhakikisha mkulima anapata faida stahiki na Taifa linakuwa na uwezo wa ndani wa kuzalisha viuatilifu salama kwa mazingira.