Na Jackline Martin, TimesMajira Online
Zaidi ya wajasiriamali 195 watembelea banda ya SIDONa Mwandishi wetu Wajasiriamali zaidi ya 195 kutoka mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani wameshiriki ndani ya Banda la SIDO wakijumuisha wajasiriamali wa programu maalumu ya ubunifu na kuongeza tija kwenye uzalishaji.
Aidha mwitikio huo wa wajasiriamali na wananchi kutembelea Banda la SIDO umeonyesha mafanikio ya huduma zinazotolewa na SIDO na uhitaji wa huduma hizo kwa wale ambao hawajafanikiwa.
Hayo yamesemwa leo na Mkurugenzi Mkuu SIDO Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Banda lao la SIDO wakati wa Maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya biashara (Sabasaba) yaliyoenda sambamba na kaulimbiu isemayo ‘Tanzania ni Mahali sahihi pa Uwekezaji na Biashara ‘
“Maonyesho haya ni fursa ya kipekee ya kuonyesha na kutambulisha bidhaa na mashine zinazozalishwa na viwanda vidogo na vya kati hapa nchini ikiwemo vituo vya SIDO vya Teknolojia vinavyozalisha mashine na vipuri mbalimbali “
Aidha Mhandisi Prof. Mpanduji amezitaja aina mbalimbali za Teknolojia zenye kuongeza thamani ya mazao mbalimbali ambazo zinapatikana ndani ya Banda lao la SIDO.
“Ndani ya banda la SIDO kipekee mtaweza kuona aina mbalimbali za mashine za mnyororo wa thamani wa mazao ya kilimo, mifugo, misitu, madini zikiwemo za mashine za kusindika mazao ya mahindi, matunda, asali, alizeti, mpunga, karanga, Mchikichi, muhogo, korosho n.k”
“Pia zitakuwepo mashine za utengenezaji wa bidhaa za ngozi, usindikaji wa maziwa, utengenezaji sabuni, mishumaa, chaki, ujenzi, upuraji wa nafaka, mashine za vyakula vya mifugo, ukataji nyasi n.k” Amesema Mhandisi Prof. Mpanduji.
Mhandisi Prof. Mpanduji amesema Bidhaa nyingine ni za usindikaji vyakula kama vile viungo vya chakula, uyoga, samli, mafuta ya alizeti, mboga za majani zilizokaushwa na asali kutoka Tabora.
Mbali na hayo Mhandisi Prof. Mpanduji amewakaribisha wananchi wote kwenye maonesho ya nne ya kitaifa yatakayofanyika mkoani Njombe kuanzia tarehe 21 hadi 31 Octoba 2023 yanayoenda sambamba na kaulimbiu isemayo ‘ Pamoja tujenge viwanda kwa uchumi na ajira endelevu’
“Maonesho haya ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kutathimini, kupenda na kutumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vidogo na vya kati nchini ili kuongeza tija ya uzalishaji katika viwanda na ajira endelevu”
More Stories
Mzumbe yaanika siri ya shahada udaktari wa heshima kwa Samia
Kujenga ofisi ya kisasa,akipewa ridhaa ya Uenyekiti
Ushiriki wa Rais Samia G20 wainufaisha Tanzania