Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mbeya imesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitano,imefanikiwa kuwakopesha wananchi kiasi cha zaidi ya bilioni 4,ikiwa ni jitihada za Serikali kuhakikisha wanaepuka na mikopo umiza.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya Mbeya,Agnes Elikunda,wakati halmashauri hiyo ilipokabidhi hundi ya mfano ya zaidi ya shilingi milioni 700 kwa vikundi vya wajasiliamali wakiwemo maofisa usafirishaji 32 wanaofanya shughuli mbalimbali za kiuchumi .

Hata hivyo Elikunda,amevitaka vikundi hivyo kuwa waaminifu na kurejesha kwa wakati ili wananchi wengine waweze kunufaika.Ambapo vikundi hivyo vimepata mikopo kwa kipindi cha robo pekee.
Mgeni rasmi .katika hafla hiyo ni aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini Oran Njeza, ambapo amesema mikopo hiyo ni takwa la kikanuni ambalo Serikali ilishajiwekea kurejesha fedha hizo kwa wananchi kwa njia ya mikopo ya bila riba na kwamba CCM iliahidi kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Kwa upande wake Beatrice Ngutu,akimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya,amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kwenda kuitumia vizuri kuinua uchumi wao, familia zao na taifa kwa ujumla kwani mikopo hiyo sio zawadi.

Aron Sote ni Ofisa Tarafa ya Isangati akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Solomon Itunda, amesema wako baadhi ya watu wakipata pesa huzitumia kwa mambo yasiyo ya msingi na lazima na kuwa watakaobainika kutumia mikopo hiyo vibaya watachukuliwa sheria.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mbeya Vjijini,Akimu Mwalupindi, ameipongeza Halmashauri hiyo kwa kuhakikisha mikopo hiyo inatolewa.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi