Na Mary Margwe, Timesmajira Online,Simanjiro
Zaidi ya bilioni 19,zimetengwa kwa ajili ya kujenga barabara na madaraja katika Halmashauri zote za Mkoa wa Manyara,ili kukabiliana na changamoto ya ubovu wa miundombinu hiyo.
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga,wakati akikagua zahanati mpya ya kitongoji cha Oltotoi,kijiji cha Kimotorock, Kata ya Loiborsiret, wilayani Simanjiro mkoani humo,ambapo amesema kufuatia changamoto za ubovu wa barabara ,kiasi hicho cha fedha zimeidhinishwa kwa ajili ya kukamilisha hilo, kinachosubiriwa ni mvua tu ikatike ili wakandarasi waingie barabarani.

” Tangu mwaka jana mwezi wa 9-10 mvua zilianza kuonyesha hadi hivi sasa,tumepewa fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa barabara pamoja na madaraja,”.
Sendiga amesema, barabara mbaya zaidi ni za wilaya ya Mbulu, Hanang’ na Kiteto, huku barabara za Simanjiro zina nafuu ukilinganisha na hizo , hivyo amewataka wananchi waendelee kuwa na subira na uvumilivu ili mvua zikate , kipindi cha jua kikianza wakandarasi wataanza kazi.


More Stories
Mke wa Rais wa Finland atembelea Makumbusho ya Taifa
Lulida ataka viwanda vilivyofungwa vifufuliweÂ
WMA yahakiki vipimo asilimia 99 ya lengo