June 14, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Zaidi ya bilioni 10.5 zatumika kutekeleza miradi ya maendeleo Kata ya Endiamtu 

Na Mary Margwe, Timesmajira Online-Simanjiro 

Katika kipindi cha miaka mitano Serikali imepeleka zaidi ya bilioni 10.5,kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali  ya maendeleo  Kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro mkoani Manyara.

Diwani wa Kata ya Endiamtu wilayani Simanjiro Mkoani Manyara,Lucas Chumba,akizungumza na wananchi wa kata hiyo  katika mkutano wa hadhara uliofanyika kitongoji cha Endiamtu, amesema  utekelezaji wa Ilani ya CCM katika kipindi cha 2020-2025, Serikali ilipeleka fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kata hiyo.

Chimba amesema,mradi wa ujenzi wa jengo la kitega uchumi la ‘Tanzanite City’ ( soko la madini ya Tanzanite) wenye thamani ya bilioni 5.4, unaendelea kwenye Kata hiyo.

Mradi mwingine ni wa maji wenye thamani  ya zaidi ya bilioni 4.3, afya milioni 300.6 na  sekta ya elimu msingi na sekondari wenye zaidi ya milioni 500.

Mmoja wa wananchi wa Kata hiyo, Aponary Massawe amesema, katika kipindi hicho cha utekelezaji  wa ilani ya uchaguzi kupitia Diwani huyo Kata hiyo imeweza kupata maendeleoabalimbali ikilinganishwa na kipindi kilichopita.

Huku akitolea mfano jitihada alizofanya Diwani huyo Ikiwa ni pamoja na kutengeneza madawati  87 yenye thamani ya milioni 6.96, hali iliosaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madawati.

Naye  Salama Rajabu amesema, ujenzi unaoendelea wa jengo la soko la madini ya Tanzanite utakapokamilika wananchi wataweza kubadilisha maisha yao kupitia uwekezaji wake katika kufanya biashara mbalimbali za ujasiliamali na kujiongezea kipato.