Aliyekuwa kocha wa Yanga Mwinyi Zahera ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Ufundi ndani ya Gwambina FC, amefunguka kuwa klabu hiyo imepata mtu sahihi kwa kukamilisha usajili wa winga Mkongo, Tuisila Kisinda.
Zahera ameongeza kwamba Yanga wamepata mtu sahihi kutokana na winga huyo kuwa na faida nyingi uwanjani ikiwemo kufunga, kupiga chenga, kupiga mipira ya vichwa na pia atakuwa mrithi sahihi wa pengo la winga Mghana, Bernard Morrison aliyekwenda Simba.
Yanga walitangaza kumalizana na Tuisila aliyekuwa anaichezea AS Vita ya DR Congo sambamba na kiungo mkabaji Tonombe Mukoko.
Zahera amesema kwamba Kisinda ni mchezaji mzuri na atawasaidia sana Yanga baada ya kumsajili kutokana na matumizi mengi aliyonayo winga huyo.
“Tuisila ni mchezaji mzuri na atawasadia sana kwa sababu ni winga mwenye mbio na ambaye anaweza kufanya maamuzi, Yanga wamempata ni jambo zuri kwao.
“Kwangu ni mzuri sana kumzidi Morrison (Bernard) na anaweza kufanya kazi zaidi ya moja uwanjani, anaweza kufunga, kupiga chenga, anaweza kupiga mipira ya vichwa,” alimaliza Zahera.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025