December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Young Lunya akanusha kutoka na Uwoya

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MSANII wa muziki wa Bongo fleva, Young Lunya amekanusha madai ya stori zinazosemekana kwamba anatoka kimahusiano na staa wa filamu hapa nchini Irene Uwoya kuwa si za kweli, kwani zingekuwa na ukweli ingeshajulikana.

Akizungumzia madai ya stori hizo zinazoendelea kwenye mitandao ya kijamii Young Lunya amesema, ingekuwa ni kweli basi ingeshajulikana, kwa kuwa mahusiano sio kitu cha kufichika.

Hiyo sio mara ya kwanza kwa Young Lunya kusemekana kwamba ana mahusiano na mastaa wa kike kwani kipindi cha nyuma zilitoka stori zinazosema ana-date na Mimi Mars pamoja na Barbiemia.