Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Mawasiliano hapa nchini Yas, imezidi kujiimarisha katika kuboresha huduma zake kwenye sekta ya utalii kuhakikisha kila mmoja anapata huduma iliyo bora.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Kitengo Cha Mafunzo kwa wateja wakubwa na Serikali, Anatori Lelo katika maonesho ya Utalii maaraufu kama ‘Kill Fair’ yaliyofanyika jijini Arusha hivi karibuni.
Akizungumza katika maonesha hayo, Anatori Lelo amewaasa wananchi wa Jiji la Arusha na maeneo mbalimbali waliotembelea maonesho ya Utalii maarufu kama Karibu Kill Fair ili kupata huduma mbalimbali zikiwemo za kimtandao Kutoka kampuni ya Mawasiliano Tanzania.
Lelo amesema,wao kama YAS wameshiriki maonesho hayo Ili waweze kutoa huduma mbalimbali za kimtandao kwa wananchi na wageni wanaotembelea eneo hilo.

‎”Tumekuja kushiriki kwenye maonesho ya ‘Kill Fair’ kwa sababu yanawaleta pamoja washiriki wengi hasa Kutoka sekta ya utalii ambapo na sisi YAS tupo kwenye mnyororo huo wa thamani kwa kusapoti utalii kupitia mtandao wetu.
“Sisi tunatoa huduma nyingi katika hoteli, Makampuni katika ‘connectivity na mawasiliano,kwa hiyo tumeamua kuja kushiriki kukutana na wateja wetu,” amesema Lelo.
‎Aidha amesema, katika maonesho hayo wanaelimisha jamii kuhusu matumizi ya mtandao hasa wa YAS lakini pia kutatua changamoto za kimtandao zinazowakabili wananchi.
Hata hivyo amesema, wameendelea kuboresha mtandao huo haswa kwenye upande wa Intaneti vifurushi vya malipo ya kabla na wakati

More Stories
ZOLA yajipanga kupeleka Nishati Safi kwa Watanzania, yaunga Mkono Juhudi za Rais Samia
Kiongozi wa Mwenge awataka RUWASA kukamilisha mradi wa maji kwa wakati Kilindi
Balozi Nchimbi aongoza waombolezaji kumuaga Mzee Mongella