Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Onlinee
KAMPUNI ya Mawasiliano hapa nchini, Yas imekabidhiwa Tuzo ya mbio za CRDB Marathon 2025, kutokana na udhamini qa mbio hizo pamoja na ushiriki uliotukuka
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Yas Kanda ya Dar Kaskazini, Aidan Komba jinsi walivyoshiriki kwa moyo wa dhati kudhamini mbio hizo.
Tuzo hiyo walitunukiwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Tulia Ackson, mara baada ya kuhitimisha mbio za CRDB Marathon, zilizofanyika hivi karibuni jijini Dar se Salaam.

“Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akikabidhi tuzo kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano Yas – Kanda ya Dar es Salaam Kaskazini, Bw. Aidan Komba, kama sehemu ya kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kufanikisha maandalizi ya mbio za CRDB Marathon zilizofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni”.
“Tulitunukiwa tuzo maalumu ya udhamini na ushiriki wa mbio hizi. Tunashiriki katika kuboresha jamii inayotuzunguka sio tu kwa kudhamini matukio kama haya bali pia kwa kusambaza huduma bora ya mtandao kwa kasi ya 4G na 5G.
“Lakini pia, na kubuni suluhishi za kifedha mbalimbali ili kurahisisha maisha ya kila siku ya watanzania.
Kwa upande wake Benki ya CRDB, iliipongeza Yas kwa kusimama vizuri na Benki hiyo kwenye msimu wa sita qa CRDB Marathon.
“Ushirikiano huu, umetufanikisha kusambaza tabasamu kwa maelfu ya watu na kuandika historia nyingine kubwa,”.

More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako