Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya mawasiliano hapa nchini, Yas imeonesha dhamira yake ya dhati katika kuboresha ustawi wa jamii kwa kutoa msaada wa vifaa tiba muhimu katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze, mkoani Pwani.
Mpango huo, uliongozwa na Mkurugenzi wa Kanda ya Pwani Kusini, Fadhila Saidi ambaye alimkabidhi vifaa hivyo, Ramadhan Possi, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo.

Msaada huo, ulijumuisha vitanda vya wagonjwa 15, mashuka 15, mizani ya watoto 2, kifaa cha kupasha joto watoto wachanga 1, mifuko ya kolostomi 100 na meza za Mayo 5.
Aidha, msaada huo ulitolewa kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze na kuhudhuriwa na viongozi wa Halmashauri, wafanyakazi wa Yas na Mixx pamoja na wageni waalikwa.

“Kwa Yas, kutoa si tendo tu-ni taswira ya dhamira yetu ya kweli. Tunaamini kuwa kwa kuviwezesha vituo vya afya, tunajenga jamii imara na zenye afya bora.
“Kila mchango ni hatua ya kuanzia tulipo, kuelekea kesho yenye matumaini,”.


More Stories
Bilioni 7 kuwainua vijana 308 sekta ya uvuvi
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako