January 13, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Yanga yaendeleza ubabe Kaitaba

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

KIKOSI cha timu ya Yanga kimefanikikiwa kuendeleza ubabe katika uwanja wa Kaitaba, Bukoba baada ya kuwafunga wenyeji wao, Kagera Sugar 1-0 katika mchezo wao wa raundi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) uliochezwa leo jioni .

Goli hilo pekee katika mchezo huo lilifungwa dakika ya 71 na mchezaji Mukoko Tonombe akimalizia pasi na mchezaji wenzake Tuisila Kisinda.

Ushindi huo umewaweka Yanga kileleni mwa msimamo wa Ligi baada ya kufikisha pointi saba wakishinda mechi mbili na kutapa sare moja.

Kabla ya goli hilo timu zote zilionekana kucheza kwa kujihami zaidi lakini wakifanya mashambilizi kadhaa ambayo hayakuweza kuleta madhara jambo lililofanya kwenda mapumziko bila kufungana.

Lakini mara baada ya Yanga kupata goli hilo, Kagera Sugar walibadili mfumo wa mchezo wa kujihami lakini wakishambulia zaidi jambo lililoongeza kasi ya mchezo.

Licha ya kusaka goli la kusawazisha lakini bahati haikuwa kwao kwani Yanga walilinda goli lao na hadi dakika 90 zinamalizika Kagera hawakuweza kusawazisha goli hilo.

Mchezo uliotangulia leo mchana, Tanzania Prisons ilipata ushindi wa kwanza baada ya kuwachapa Namungo FC 1-0, bao pekee la Gasper Mwaipasi dakika ya 47 Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Mbali na mchezo huo, Maafande wa Tanzania Prisons jana wamefanikiwa kuchukua alama tatu katika uwanja wao wa nyumbani wa Nelson Mandela, Sumbawanga baada ya kuwafunga Namungo goli 1-0 lililofungwa dakika ya 47 na Gaspar Mwaipasi.