Cedric Kaze raia wa Burundi ndiye anayetajwa kuwa kocha mpya wa Yanga akitokea kule Amerika ya Kusini ambako anafanya kaziBado wanayanga wanasubiri ujio wake, uongozi wa Yanga ukibainisha kuwa atawasili wiki hii tayari kuanza majukumu yake.
Taarifa zaidi zimebainisha kuwa kilicho mchelewesha Kaze ni kusubiri majibu ya vipimo vya COVID-19 ili apatiwe vibali asafiriMkurugenzi wa Uwekezaji GSM.
Mhandisi Hersi Said amesema kocha huyo anaweza kuwasili kati ya kesho au IjumaaLakini pamoja na kuchelewa, Kaze ameanza majukumu yake kwa ushirikiano na kocha msaidizi Riedoh Berdien ambapo inaelezwa ametuma program za mazoezi ya awali ambayo yanasimamiwa na RiedohMwishoni mwa wiki hii Yanga inaweza kumtambulisha Kaze sambamba na wachezaji wengine waliosajliwa kwenye ufunguzi wa msimu wa wiki ya Mwananchi kule mkoani Dodoma siku ya Jumamosi August 22, 2020
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025