Na Mwandishi Wetu, Timesmajira
Klabu ya Yanga SC, imetangazwa kuwa Mablozi wapya wa Kampeni ya kupinga na kutokomeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.
Akitangaza hilo leo mbele ya Waandishi wa Habari kwenye ukumbi wa Wizara TACAIDS Posta, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum. Dkt. Dorothy Gwajima amesema anaamini klabu hiyo itakuwa balozi mzuri kutokana na kuwa na mashabiki wengi hapa nchini.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwatambulisha rasmi Klabu ya Yanga SC, kuwa Mabalozi wa kampeni ya kupinga na kutokeza mmomonyoko wa maadili na unyanyasaji wa kijinsia na watoto, amesema Dkt. Gwajima.
Naye Rais wa Yanga SC, Hersi Ally Said amesema klabu ya Yanga imelipokea hilo kwa mikono miwili hivyo hawana budi kuungana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima katika kampeni hiyo.
“Napenda kutoa rai kwa vilabu vya Simba SC, Azam FC, KMC na vingine vyote kuunga mkono kampeni hii, kampeni hii siyo mashindano ya kibiashara sote kwa pamoja tuungane na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima kutokomeza changamoto hizi kubwa na kuilinda jamii yetu,” amesema Hersi Ally Said.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania