Na Judith Ferdinand,TimesMajira Online, Mwanza
Jumla ya wafanyakazi wa nyumbani 165, waliokumbana na ukatili wameokolewa na shirika la WoteSawa kwa kipindi cha Januari mwaka 2022 hadi sasa.
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Nyumba salama wa shirika la WoteSawa Jacqueline Ngalo,wakati wakiadhimisha siku ya wafanyakazi wa nyumbani dunia pamoja na siku ya mtoto wa Afrika,ambayo huadhimishwa Juni,16 mwaka huu yaliofanyika katika makao makuu ya shirika hilo jijini Mwanza.
Ngalo ameeleza kuwa,shirika hilo limefanikiwa kuwaokoa wafanyakazi hao wa nyumbani na kuwapa huduma mbalimbali kama vile malazi,chakula,msaada wa kisaikolojia, matibabu na msaada wa kisheria.
“Kati ya hao 86, wamerejeshwa na kuunganishwa na familia zao kwa takwimu hizi ni wazi kuwa ukatili na unyanyasaji kwa wafanyakazi wa nyumbani ni tatizo kubwa na hivyo sote tunapaswa kuchukua hatua madhubuti kukabiliana na jambo hilo,”ameeleza Ngalo.
Sanjari na hayo ameeleza kuwa bado wafanyakazi wa nyumbani wanakumbana na changamoto mbalimbali zikiwemo kuajiriwa katika umri mdogo,kutokulipwa mishahara stahikinkwa wakati.
Pamoja na kufanyakazi bila mikataba ya maandishi,kutopewa haki ya likizo na mapumziko mengine huku wakitendewa ukatili na unyanyasaji.
“Tutambue kuwa haya yote yana toke kwa sababu hakuna sheria mahususi yenye kulinda haki za mfanyakazi wa nyumbani kulingana na mazingira halisi ya kazi hiyo,”.
Aidha ameeleza kuwa kuridhiwa kwa mkary wa kimataifa wa wafanyakazi wa nyumbani Na.189/2011 na kuwepo kwa sheria mahususi kwa ajili ya wafanyakazi hao nchini kutasaidia kuimarisha mazingira yenye staha kwa kundi hilo na kuwezesha usimamizi mzuri wa kisheria kwa masuala yanayohusu wafanyakazi hao.
“Serikali iridhie mkataba wa kimataifa wa kazi za staha kwa wafanyakazi y nyumbani namba 189/2011 na kuweka sheria maalumu itakayosimamia ajira ya kazi nyumbani,pia itekeleze kikamilifu sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 sambamba na mkataba wa Shirika la Kazi la Kimataifa (ILO) Na.138/1974 unaoweka katazo la ajira kwa watoto chini ya umri wa miaka 14,”.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi,Ofisa Kazi Mkoa wa Mwanza Betty Mtega,ameeleza kuwa ni kosa kisheria kumuajiri mtoto aliteye chini ya umri wa maika 14 pia ni kumnyima haki yake ya elimu.
“Kauli mbiu duniani kote ni Hakuna usawa wa kijamii bila kuwa na kazi za staha kwa wafanyakazi wa nyumbani kwa mujibu wa kauli mbiu hii waajiri wanaaswa kuwalipa wafanyakazi wao wa nyumbani kwa kuzingatia kima cha chini cha mshahara kama iluvyoainishwa katika amri ya kima cha chini cha mshahara ambayo ni 60000 kwa wafanyakazi wa nyumbani wanaoishi kwa muajiri na 120000 kwa wasioishi kwa muajiri,” ameeleza Mtega.
Kwa upande wake mmoja wa mabinti wafanyakazi wa nyumbani Neema Ishengoma amewahimiza waajiri wao wawapende na wasiwabague huku jamii iwape kipaumbele kwa kutoa taarifa na kuchukua hatua pindi watoto wafanyakazi wa nyumbani wanapofanyiwa vitendo vya ukatila na unyanyasaji.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa