Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Waajiri wa wafanyakazi wa nyumbani wametakiwa kuhakikisha wafanyakazi wao wanakuwa katika mazingira salama pamoja na kuwapa elimu ya afya ya uzazi ili kuwakinga wasiweze kupata maambukizi ya VVU.
Ambapo takwimu zinaonesha asilimia 40 ya maambukizi mapya ya VVU ni vijana wa rika balehe na kati yao asilimia 80 ni vijana wa kike.
Wito huo umetolewa na Meneja wa Nyumba Salama kutoka shirika la kututea haki za wafanyakazi wa nyumbani la WoteSawa Jacqueline Ngalo,wakati akizungumza na timesmajira online mara baada ya maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani ambayo uadhimishwa kila ifikapo Desemba mosi kila mwaka,ambapo kwa mwaka huu kimkoa yamefanyika uwanja wa Mirongo wilayani Nyamagana yenye kauli mbiu isemayo “Imarisha Usawa”
Ngalo ameeleza kuwa,WoteSawa wamekuwa wakihamasisha waajiri wahakikishe kwamba wanaweka mazingira safi na salama kwa wafanyakazi wao wa nyumbani.
Pamoja na kuhakikisha wanafanya kazi katika mazingira ambayo hayatapelekea kupata ukatili hasa wa kingono unaoweza kuchangia wao kupata maambukizi ya VVU kwani wengi wao wamepata ukatili wa kingono na wakati mwingine taarifa hazifiki kwenye mamlaka husika.
Ameeleza kuwa,asilimia kubwa ya wafanyakazi wa nyumbani ni wasichana wenye umri wa miaka kati ya 13-17,ambao wapo wengi sana kwenye ajira ambazo siyo salama,lakini pia sheria inasema kuwa mtu asiajiri mtoto chini ya umri wa miaka 14,ingawa wapo hadi wa miaka 8 na 9.
Ambapo waajiri wengi hawachukui nafasi yao katika kuwapa elimu ya afya ya uzazi wafanyakazi wao wa nyumbani hali inayosababisha wao kuwa katika hatari ya kupata madhara mbalimbali ikiwemo maambukizi ya VVU.
“Sisi WoteSawa,tumekuwa tukifanya kazi na wafanyakazi wa nyumbani moja kwa moja kwa kuwapa elimu ya afya ya uzazi kwa sababu wanapotoka kijijini kuja mjini kufanya kazi za nyumbani wanakuwa hawana elimu ya namna gani wanatakiwa waishi ili kuepuka madhara mbalimbali ikiwemo ya maambukizi ya VVU,”ameeleza Ngalo.
kuzingatia kuwa na staha kwa wafanyakazi wa nyumbani pamoja na kupinga usafirishaji haramu wa binadamu hasa watoto kwa sababu watoto wengi wamekuwa wakusafirishwa na kwenda kutumikishwa kwenye kazi za nyumbani na biashara ya ngono.
ambao itapelekea kupata magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya zinaa, Ukimwi na mengineyo na kupata mimba wasizozitarajia ambayo utaleta madhara makubwa sana.
Pia ameeleza kuwa, jamii hasa waajiri kuhakikisha kwamba kunakuwa na mazingira ya afya na usalama wa mfanyakazi wa nyumbani kwani inachangia usalama wa nyumbani kwako.
Mwajiri aone kuwa mfanyakazi akiwa salama na familia inakuwa salama,wakati mwingine wafanyakazi wa ndani wamepewa jukumu la kuwahudumia wagonjwa wakiwemo waathirika wa VVU/Ukimwi bila kupewa zana yoyote ya kujikinga wala kupewa elimu yoyote ya kujikinga kuwa ni kwa namna gani wanaweza kuwahudumia wagonjwa hao bila wao kupata madhara.
“Kwaio sisi tunahamasisha waajiri kuhakikisha kwamba wafanyakazi wanakuwa salama kwa sababu pamoja na mambo mengine anaendelea kuhudumia familia hivyo asipo kuwa salama maana yake usalama wa familia utakuwa ni mdogo ndio maana tunasema mfanyakazi wa nyumbani salama, familia salama,”na kuongeza kuwa
“Kama wakipewa majukumu ya kuhudumia wagonjwa wenye maambukizi yoyote basi ni vyema wakapewa vitu kwa ajili ya kujikinga mfano kuvaa barakoa au glovisi zitakazowasaidia kujikinga na maambukizi lakini pia kuchukua jukumu la kuzungumza nao kuhusiana na suala la afya ya uzazi,”ameeleza Ngalo.
Sanjari na hayo ameeleza kuwa kauli mbiu ya maadhimisho hayo inasisitiza kuimarisha usawa,hivyo ameomba kila mmoja kuwa jicho kwa mwenzie na kuhakikisha mfanyakazi wa nyumbani anatambulishwa katika mamlaka ya serikali za mitaa.
Kama yalivyo makundi mengine kuhakikisha wanapata usawa kwa serikali na wadau mbalimbali kuhakikisha wanawaweka katika mipango yao sababu wafanyakazi wa nyumbani wana umuhimu katika kuchangia maendeleo ya taifa kwa kusaidia wengine waweze kufanya shughuli za kiuchumi.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba