Na Grace Gurisha, TimesMajira Online
WIZARA ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeshatoa maagi TVzo ya kufanya mapitio ya sheria na sera ya Tume ya Taifa Sayansi na Teknolojia (Costech) ili kuhakikisha kwamba inaendana na bunifu zinazoendelea hivi sasa.
Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri, Juma Kipanga wakati alipotembelea banda la Costech katika maonesho ya 46 ya Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam kwa niaba ya Waziri wa wizara hiyo.
Amesema wakati sheria hiyo inaanzishwa kulikuwa hakuna eneo la ubunifu ndani yake ndiyo maana wanataka kufanya mapitio hayo, kwa sababu wanataka bidhaa zinazobuniwa ziweze kutatua changamoto hapa nchini.
“Tumepiga hatua kama tunavyoona tunatengeneza bidhaa mbalimbali kupitia bunifu zetu za ndani , tulichosisitiza ni kuhakikisha bunifu zao zinawafaidisha wao wenyewe, lakini pia zinaweza kutengeneza ajira kwenye jamii,”amesemaÂ
Kipanga Hata hivyo, Kipanga amesema wameona wabunifu mbalimbali waliyoendelezwa na Costech, kabla ya hapo walikuwa na mfuko wao na pia kuna mashindano yanaitwa makisatu.
“Vyombo vyote hivi vimeundwa kuhakikisha kwamba bunifu pamoja na tafiti zinaweza kukuzwa na kuendelezwa ili badae ziwe bidhaa,” amesema Kipanga
Kipanga ametoa rai na wito kwa Costech kuendelea kufanya kazi na kushirikiana kwa sababu Taifa hili litajengwa na watanzania wenyewe na lengo la bunifu hizi ni kuhakikisha zinatatua changamoto.
“Tutatumia bunifu zetu za ndani kwa sababu ni rahisi kupata bidhaa inayoweza kutatua changamoto kwa bei rahisi na pia inaweza kutumika kwa urahisi,”amesema KipangaÂ
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato