November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya ujenzi,TBA wazindua majengo yenye thamani ya bilioni 10.3

Na Irene Clemence Timesmajira online

WIZARA ya Ujenzi na Uchukuzi na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), umezindua majengo mawili yenye thamani ya bilioni 10.3 kwa ajili ya makazi ya watumishi wa umma katika eneo la Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsular.

Akizindua majengo hayo mapema leo hii Machi 29,mwaka huu Jijini Dar es Salaam , Waziri wa wizara hiyo, Profesa Makame Mbarawa amesema kukamilika kwa mradi huo ni kutokana na serikali ya awamu ya sita kutoa fedha kwa wakati.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Ujenzi akikata utepe kuashiria uzinduziwa wa nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopo Magomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa katika jengo la ghorofa lililojengwa eneo la Magomeni Kota limegharimu billioni 5.6 na jengo lingine limejengwa kwa zaidi ya bilioni 4.

Ambapo amesema gharama ni nzuri kwa hiyo TBA iendelee kusimamia ubora na gharama.

“Mradi huu umetumia bilioni 10.3 naomba watakaopata nafasi ya kuishi katika nyumba hizi wazitumie vizuri ili zibaki kwenye ubora wake na kuzingatia masharti ya mkataba ikiwemo kulipa kodi kwa wakati,” na kuongeza kuwa

“Hatutaki baada miezi mitatu nyumba ziwe imejaa moshi, TBA kama kuna mpangaji haendani na masharti mtoeni mumuweke mwingine pia mmenifurahisha kuweka kitasa janja hii itasaidia kodi kulipwa kwa wakati,” alidai Profesa Mbarawa.

Amesema Serikali itaendelea kuiongezea mtaji TBA ili nyumba za kuwapangisha watumishi wa umma ziweze kujengwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa ubora unaostahili.

Aidha, amesema Serikali imeruhusu ushilikishwaji wa sekta binafsi katika ujenzi wa miradi mbalimbali kwa hiyo anatoa wito kwa watanzania wote ambao wapo tayari kushirikiana na wakala hao kwa sababu kibali kimeshatolewa.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati za Bunge ya Miundombinu, Sulemani Kakoso, amesema wameona ubora uliyojengwa kwenye majengo hayo, kwa hiyo watakaopata nafasi ya kukaa humo wanatakiwa wazitunze.

Pia, amesema amefurahishwa na kitendo cha nyumba hizo kuwekewa kitasa janja ambacho kitarahisisha ukusanyaji wa kodi, kwa hiyo kama mpangaji akipitiliza muda wake basi mlango wake unajiloki, kwa hiyo mpango huo ni nzuri.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa akifurahia jambo naMtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Arch. Daud Kondoromara ya kuzindua nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopoMagomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar esSalaam.
Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa akizungumza wakati wa uzinduzi wa majengo hayo leo Machi 29 Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Watumishi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), wakimsikilizaWaziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani)wakati alipozindua nyumba za makazi za watumishi wa umma zilizopoMagomeni Kota na Canadian Village Msasani Peninsula -Masaki jijini Dar esSalaam.