Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wizara ya Nishati na kampuni ya DP World ya Dubai zimesaini hati ya makubaliano ya ushirikiano katika kuendeleza miundombinu ya kupokea na kuhifadhia mafuta na gesi itakayojengwa nchini Tanzania.
Utiaji saini huo umefanywa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya DP World ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bandari, Bohari na Eneo Huru la Kibiashara – Dubai, Sultan Ahmed Bin Sulayem.
Mradi uliolengwa katika Hati ya Makubaliano husika ni kuendeleza miundombinu ya kitaifa iliyo bora na ya kisasa ya kupokea na kuhifadhi mafuta na gesi ambayo itatumika katika kuboresha sekta ya mafuta na gesi nchini na katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Tukio hili lilifanyika tarehe 27 Februari, 2022 katika Kikao cha Kibiashara kilichofanyika huko Dubai – Umoja wa Falme za Kiarabu.
More Stories
Wagombea CHADEMA wakipewa ridhaa,watakuwa wawazi
TTCL yafanya maboresho katika huduma zake
HGWT yawataka wazazi na walezi kulinda watoto dhidi vitendo vya ukatili