Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wizara ya Madini na Taasisi zake inaendelea na ushiriki wake katika Maonesho ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, yanayoendelea katika Viwanja vya Maisara, Zanzibar.
Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini zinazoshiriki ni pamoja na Tume ya Madini, Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania(GST), Taasisi ya Uhamasishaji Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Kituo cha Jemolojia Tanzania (TGC) pamoja na Chama cha Wanawake Wachimba Madini Tanzania (TAWOMA)
Maonesho hayo yenye kaulimbiu inayosema, Tumia Bidhaa za Tanzania, Jenga Tanzania yalianza tarehe 03 Desemba, 2021 yanatarajiwa kumalizika tarehe 09 Desemba, 2021
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato