December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya Kilimo kuja na Teknolojia itakayodhibiti Sumukuvu

Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbeya

KATIKA kudhibiti sumukuvu ,Wizara ya Kilimo imekuja na teknolojia mbalimbali zinatakazoweza kudhibiti sumukuvu hiyo ikiwemo viuatilifu pamoja na teklojia nyingine katika kuhifadhi mazao tangu wakati wa kilimo mpaka kuhifadhi mazao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mtaalam kutoka wizara ya Kilimo, Hilda Shegembe wakati akizungumza na waandishi kwenye maonyesho ya sikukuu ya wakulima Nane nane ambayo kitaifa inafanyika mkoani Mbeya.

Shegembe amesema kuwa moja ya teknolojia hiyo ni kipukucho mahindi ambayo ni teknlojia rahisi inayoweza kudhibiti sumu kuvu na bei yake ni rahisi kwa mkulima yeyote anaweza kumudu.

“Hiki ni kwa ajili ya wakulima wadogo ambao wamekuwa wakipukucha mahindi yao kwa kuyapiga,hii ni hatari kwa usalama wa chakula kwa sababu wakati wa kuyapiga yapo yanayopasuka,hayo yanayopasuaka husababisha wadudu wa sumukuvu kuingia katika mazao.”amesema Shegembe.

Mercy Buta ni Mtaalam Udhibiti Ubora mradi wa kuthibiti Sumukuvu (TANIPC) mradi huo unatekelezwa kwenye Mikoa 10 katika halmashauri 18, lakini pia unatekelezwa Zanzibar katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Aidha Butta amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuimarisha usalama wa chakula ndani na nje ya nchi pamoja na afya ya jamii .

“Kwa hiyo tupo katika maonyesho haya hapa Mbeya kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu sumu kuvu ambayo ni sumu inayosababishwa na kuvu (fangus) .”amesema Butta

Kuhusu madhara ya sumu kuvu Mtaalam huyo alisema,madhara ya sumu kuvu ni halisi na kwamba mtu akila kwa muda mrefu chakula chenye sumu matokeo yake ni kupata kansa .

“Kansa zinapzoripotiwa asilimia 30 inaweza kuwa zinasbabishwa na sumu kuvu, ndio maana mradi wa kuelimisha jamii umekuja ili kukabiliana na suala hilo .”amesema.

Naye Mtaalam kutoka Wizara hiyo Pendo Nsanya alisema teknlojia nyingine ni ya kipima unyevu ambacho kinatumika kwa kuoneakana kwa rangi ambapo kifaa hicho (kadi) humsaidia mkulima kujua kama mazao yake yamekauka ndipo ayahifadhi badala ya kuhifadhi yakiwa mabichi na hivyo kusababisha sumukuvu kuingia katika mazao.

“Kifaa hiki (Kadi) kinasaidia kuonyesha mahindi ambayo yamekauka na hivyo kuhifadhi chakula katika hali ya usalama zaidi.”