April 19, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wizara ya Habari,Utamaduni yaendesha warsha kwa wasanii

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online,Dar

MFUKO wa Utamaduni na Sanaa Tanzania umeendesha warsha maalumu yenye lengo la kuwasaidia wasanii kuandaa na kutengeneza kazi bora,ili kunufaika na milabaha ama kazi zao ndani ya nchi.

Takwimu zinaonesha kuwa tasnia hiyo inachangia pato la Taifa kwa kiasi cha asilimia 17.1 ukilinganisha na sekta nyingine nchini hivyo kuwa eneo muhimu katika kuchochea shughuli za maendeleo.

Akizungumza jijini Dar-es-Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Gerson Msigwa amesema wasanii ni nguzo muhimu katika maendeleo ya nchi hivyo inabidi kuangaliwa kwa macho mawili.

“Warsha hii ni muhimu kwa makundi haya ya wasanii ili kuweza kuwatengenezea mazingira yenye kuzifanya kazi zao ziwe zenye ubora machoni mwa watanzania kupitia serikali,” amesema Msigwa

Amesema,warsha hiyo ilijumuisha mafunzo mbalimbali ya kazi za sanaa na namna ya wasanii kupata mikopo wezeshi,ambayo itakwenda kuboresha kazi zao ama shughuli wazifanyazo kwa manufaa yao na serikali kwa ujumla.

Hata hivyo warsha hiyo ilijumuisha wasanii mbalimbali ikiwemo maigizo, wasanii bongo fleva, washairi na watunzi wa vitabu, waandishi wa script pamoja na waimbaji wa injili na wa taarabu.