Na Esther Macha,TimesMajira Online,Mbeya
NAIBU Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Mwanaidi Hamisi (Mb)amesema kuwa zipo taarifa za uvunjwaji wa maadili kwa wauguzi kutoa lugha zisizo na staha kwa wagonjwa na kwamba taarifa hizo serikali haitaweza kuzifumbia macho.
Amesema kuwa yapo malalamiko kutoka wagonjwa kutoka kwa wauguzi kwamba siri za wagonjwa zinatolewa na baadhi wauguzi kupokea rushwa na kwamba ni vizuri kila muuguzi kujitazama na kujipima upya ili kuwatendea haki wagonjwa .
Naibu Waziri wa afya amesema hayo jana wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa 48 , ,na kongamano la kisanyasi na maadhimisho ya miaka 50 ya chama cha wauguzi Tanzania (TANNA)unaofanyika kwa siku tatu katika ukumbi wa Tughimbe Jijini Mbeya.
“Pamoja na changamoto zenu za kazi zenu naomba nizungumzie suala maadili zipo taarifa kwamba kumekuwa na ongozeko la uvunjwaji wa maadili kwa wagonjwa taarifa hizi hatuwezi kuzifumbia macho ni vizuri kila muuguzi kwa nafsi yake ajitizame na kujima na kutafakari kuwa serikali hairidhishwi haya yanayosemwa na wadau wetu ambao ni wagonjwa ,ni imani yangu kuwa yote haya yaliyosemwa yatafanyiwa kazi na naamini kwamba wauguzi tuna kazi kubwa katika maeneo yenu ya kazi naombeni muwe wavumilivu na kufuata maadili na kuhakikisha kuwa taaluma yenu haihalibiliwi na kukosa sifa”amesema Naibu Waziri wa afya Mwanaidi.
Akizungumzia kuhusu wauguzi waliopo kazini Naibu Waziri Mwanaidi amesema kuwa mpaka sasa kuna wauguzi na wakunga 41,621 ndo wapo kazini na kwamba kama Taifa wanajitahidi kuongeza idadi ya wauguzi na wakunga ili kuimarisha huduma za afya kwa wananchi ili kupunguza mzigo mkubwa wa kazi kwa kila muuguzi .
Hata hivyo Naibu Waziri amesema serikali imeanza kufanyia kazi baadhi ya changamoto za wauguzi na kwamba kwa mwaka huu wa fedha 2020/2021/2022 inataraji kuajiri watumishi wa kada mbali mbali za afya wakiwemo wauguzi na wakunga wapatao 11,215 na kwamba namba hiyo si kubwa ila itasaidia kupunguza uhaba wa watumishi na kwamba serikali itaendelea kuajiri wauguzi na wakunga ili kuhakikisha kunakuwa na wauguzi wa kutosha.
Kwa upande wake Rais wa Chama cha wauguzi Tanzania (TANNA) Alexander Bulahya amesema kuwa kundi kubwa ambalo linasimamia wagonjwa ni wauguzi na wakunga ambao hawatambuliki kwani wauguzi na wakunga ndo wanatoa huduma kwa asimilia 99 huku asimilia moja t ndo wanapata usaidizi huku akitoa mfano kitengo cha mama na mtoto cha kujifungulia kina kazi kubwa sana ambazo zinahitaji usaidizi .
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Rashid Chuachua ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera ,amesema kuwa Mh Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuleta fedha kwa ajili ya kuboresha sekta ya afya Mkoa wa Mbeya .
Kwa upande wake Muuguzi Mkuu Mkoa wa Mkoa wa Mbeya ,Elesia George amesema kuwa watakikisha wanailinda taaluma ya uuguzi ambayo ni moyo wa uuguzi na yote yaliyowasilishwa yatafanyiwa kazi kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kutenga muda wa kukutana na wizara ya afya na uongozi wa wauguzi na wakunga kujadili changamoto mbali mbali za kada ya afya .
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi