November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wimbo wa KIJANISHA wazinduliwa, kuhamasisha utunzaji mazingira

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Wito umetolewa kwa jamii kuunga mkono juhudi za serikali na wadau wengine katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa haswa kwa upandaji miti lakini pia kuitikia kampeni na miradi inayoanzishwa.

Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Lead Foundation, Njamasi Chiwanga wakati wa uzinduzi wa wimbo mpya wa kijanisha mazingira ulioimbwa na Christina Shusho, John Makini, Frida Amani na Ben Paul na kwa pamoja kutangazwa kwa mabalozi wapya wa Justdiggit na wakfu wa Lead.

Njamasi amesema Mpaka sasa wameshastawisha miti zaidi ya milioni 10 katika mkoa wa Dodoma pekee ambapo walikuwa na lengo la kustawisha miti milioni 8 na kwa sasa wamenza mradi katika mkoa wa singida ambapo pia wanamalengo ya kustawisha miti milioni 8.

Kuhusu wimbo uliozinduliwa, Njamasi amesema wanaamini wimbo huo na kupitia mabalozi hao wataweza wakawafikia watu wengi zaidi na wakahamasisha ili kuweza kukomboa mazingira yetu

Njamasi amesema Mpaka kufikia 2030 wamelenga kufikia vijiji zaidi ya 1000 na kukomboa hekta zaidi ya 500,000.

Aidha amesema Mpaka sasahivi wamefikia vijiji 400 lakini pia wanamalengo mpaka kufikia 2030 waongeze vijiji vingine 1000.

Njamasi amesema kwa miaka mingi wamekuwa wakifanya kazi na msanii wa muziki wa RNB, Ben Paul kufuatia kuwa na wafuasi wengi vijana hivyo kufuatia kuongezwa kwa mabalozi hao wengine kutahamasisha vijana wengi kuongezeka na kutunza mazingira;

“Takribani miaka mitatu au minne tumekuwa tukifanya kazi zaidi na Ben Paul kama muhamasishaji na balozi wa mazingira lakini leo tulikua tunatambulisha mabalozi wengine wanna akiwemo christina shusho, John Makini, Frida Amani na Jaymond pamoja na kuwatambulisha lakini pia walikua wanatambulisha wimbo wao mpya ambao nunahamasisha utunzaji mazingira”

“Mabalozi hawa wanawafuasi wengi vijana na sisi hilo ndo kundi ambalo tunalilenga zaidi kwamba tunahitaji vijana wengi zaidi wahamasike katika kutunza mazingira ili tuweze kukomboa mazingira yetu”

Kwa upande wake Maureen anayehusika na mambo ya mazingira katika shirika la justdiggit upande wa masuala ya mawasiliano Afrika nzika amesema Kwa sasa wana mradi wa kuhamasisha kutunza mazingira lakini hivi karibuni wataongeza miradi mingine ambapo kwa sasa wanaingia mkoa wa Arusha ili Kuweza kusaidia mazingira, amesema kwa upande wao wanatumia vitu Kama kisiki hai ili Kuweza kuhamasisha mazingira

Kwa upande wake Balozi wa Mazingira Ben Paul amesema Masuala yanayohusiana na uhifadhi wa mazingira ni jukumu la watu wote hivyo kila mtu anawajibu wa kusimama kwa nafasi yake katika kuhamasisha uhifadhi wa mazingira.

Naye Balozi wa Mazingira John Makin amesema Ili kuhakikisha Dunia yetu inaendelea kuwa sehemu salama ya kuishi kwaajili yetu na kizazi kinachokuja ni jukumu la kila mmoja wetu kulivaa na kulibeba jambo hili la utunzaji wa mazingira

Mbali na hayo, Christina Shusho namesema kupata nafasi ya kuyalinda mazingira ni jukumu la kuhakikisha kwamba mazingira yetu yapo safi na salama kwa ustawi wa jamii yetu.