Judith Ferdinand, Timesmajira Online, Mwanza
Watu wawili akiwemo wifi wa marehemu washikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Flora Philimoni mwenyewe umri wa miaka 42 mkazi wa Nyamh’ongolo wilayani Ilemela.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa Desemba 20,2023 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Wilbrod Mutafungwa ameeleza kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao akiwemo wifi wa marehemu kwa tuhuma za kupanga,kuhusika na njama za mauaji ya Flora Philimoni yaliotokana na migogoro ya kifamilia ya kuwania mali.
Mutafungwa ameeleza kuwa Novemba 14,2023 majira ya saa 11 jioni huko Mtaa wa Kashishi Kata ya Nyamh’ongolo Wilaya ya Ilemela kuliripotiwa tukio la mauaji ya Flora Philimoni (42) Mkulima na mkazi wa Nyamh’ongolo aliyeuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake.
Ameeleza kuwa baada ya upelelezi na ufuatiliaji wa haraka jeshi hilo lilifanikiwa kuwakamata watu wawili akiwemo wifi wa marehemu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Amewataja watuhumiwa waliokamatwa kutokana na tukio hilo ni Elizabeth Josephat maarufu Ndakubegi(35) ambaye ndiye wifi wa marehemu na mfanyabiashara mkazi wa jijini Dar es Salaam na Faida Daud maarufu Masaba(24) mkazi wa Igoma jijini Mwanza.
Watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti na maeneo tofauti baada ya upelelezi wa kina na wote watafikishwa mahakamani.
More Stories
AZAKI yawasilisha mapendekezo yao kwa Serikali katika kuboresha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050
CP.Wakilyamba :Uvamizi maeneo ya hifadhi ya taifa katavi haukubaliki
Watu wawili wanaodhaniwa majambazi wapigwa risasi na Polisi