Judith Ferdinand, Mwanza
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linaendelea na msako mkali wa kutafuta watuhumiwa wa wizi wa watoto wawili wachanga katika maeneo mawili tofauti, walioripotiwa kuibiwa katika Wilaya ya Ilemela na Sengerema mkoani Mwanza.
Akizungumza jijini hapa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza SACP-Wilbroad Mutafungwa ameeleza kuwa katika Wilaya ya Ilemela, Mtaa wa National magharibi, mtoto jinsia ya kiume mwenye umri wa siku moja aliye zaliwa Januari 09,2023 majira ya saa 12(18:00) jioni na kuibiwa Januari 10,2023 majira ya saa Saba na dakika 30(13:30)mchana, baada ya Mama wa mtoto (jina limehifadhi,) mwenyewe umri wa miaka 23, Mkulima na Mkazi wa Sinai Nyakato kujifungua mtoto huyo na kuruhusiwa kutoka katika kituo cha afya Buzuruga kwenda nyumbani.
Mutafungwa ameeleza kuwa inadaiwa mama huyo, baada ya kufika nje ya geti la kituo hicho cha Afya alikutana na mwanamke mmoja mweupe mrefu wa wastani na kumrubuni kwa kumuomba aende nae nyumbani kwake Mtaa wa Nyakato Magharibi akapumzike.
Ampambi mama wa mtoto huyo alikubali na baada ya kufika nyumbani, mwanamke huyo alimpelekea maji bafuni ya kuoga na kumwomba aende kuoga ndipo akiwa anaoga mwanamke huyo alitoroka na mtoto na kwenda nae kusikojulikana.
Wakati huo huo Mutafungwa ameeleza kuwa katika Wilaya ya Sengerema kitongoji cha Nyankorongo Januari 14,2023 majira ya saa 2(20:00) usiku, kulipatikana taarifa za wizi wa mtoto mwenye umri wa miezi mitatu (jina limehifadhi), amabapo inadaiwa mama wa mtoto (jina limehifadhi) mwenye umri wa miaka 24, mkulima, alikwenda sokoni katika kijiji cha Nyamatale kuuza dagaa na kumwacha mtoto kwa mama yake mzazi ambaye ni Bibi wa mtoto huyo aitwaye Catherine Lubigisa.
Baadae Bibi wa Mtoto huyo naye alikwenda mashineni kusaga na kumwacha mtoto kwa dada yake aitwaye Catherine Faustine, mwenye umri wa miaka 6, mwanafunzi wa darasa la kwanza.
Aidha, Catherine akiwa hapo nyumbani na mtoto ambaye ni mdogo wake alikuja mwanamke mmoja ambae hakuweza kumtambua jina wala makazi yake na kumwambia ampatie mtoto ili amsaidie kumbembeleza na akampatia shilingi mia mbili (tsh200) ili aende kumnunulia sabuni.
Catherine alikataa, ndipo mwanamke huyo aliamua kumchukua mtoto huyo kwa nguvu na kutoroka naye kusikojulikana.
Jeshi la Polisi linaendelea na msako mkali kwa kushirikiana wananchi ili kuhakikisha linawapata watoto hao wakiwa salama na kuwakabidhi kwa wazazi wao Pia kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linawataka wazazi kuendelea kutimiza wajibu wao wa kuwatunza watoto kwa kuweka mifumo mizuri kwa kutowaacha bila uangalizi na kuacha kumwamini mtu wasiye mfahamu.
Huku linatoa rai kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka.
More Stories
CCM hakuna kulala, Nchimbi atua Tabora kwa ziara ya siku mbili
Kongamano la Uwekezaji na Biashara lafunguliwa Pwani
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi