Na Moses Ng’wat,TimesMajira Online. Songwe
WATU wenye ulemavu mkoani Songwe wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kuweka mazingira yatakayowezesha kutimiza haki yao kikatiba ya kupiga kura bila kuwepo kwa vikwazo.
Wametoa ombi hilo jana katika semina maalumu iliyoandaliwa na NEC kwa wadau wa uchaguzi mkoani hapa.
Wamesema kutokuwepo kwa mazingira rafiki kwa makundi ya watu wenye ulemavu ikiwemo uchaguzi wa mwaka huu, kunaweza kuwa chanzo cha wao kutowapata viongozi ambao watasimamia maslahi yao.
Mmoja wa walemavu hao, Martin Tembo ambaye ni mlemavu wa viungo amesema walemavu wanapaswa kupewa kipaumbele ikiwemo kuweka mazingira wezeshi yatakayosaidia wao kupiga kura bila kupata usumbufu wowote.
“Changamoto inaweza isiwe walemavu kapatiwa mahitaji yao muhimu, bali ni namna gani watashiriki kupata viongozi watakaosaidia kuelewa umuhimu wa kundi hilo na kupigania maslahi yao,” amesisitiza Tembo.
More Stories
Rais Samia amrudisha January kwa Mama,asema kilichotokea ni kumuonya
Milioni 236 kunufaisha vikundi 17 vya wanawake Minazi Mirefu
Mipango 10 kabambe ya TPA