Na Bakari Lulela,TimesMajira Online, Dar
WANAFUNZI wenye sifa za kusomea elimu ya juu washauriwa kujiunga katika chuo kikuu cha ushirika moshi kwa lengo la kupata ujuzi na maarifa kwenye masuala ya kibiashara na kujifunza maendeleo ya jamii.
Akizungumza Dar es Salaam kwenye Maonesho ya 16 ya Elimu ya Juu ya Sayansi na Teknolojia yaliyofanyika kwenye viwanja vya mnazi Mmoja, Mhadhiri wa chuo kikuu cha ushirika Moshi Dkt. Faustine Panga amesema kwamba wanafunzi wenye sifa za kujiunga na chuo chao ni wale waliopata alama (point) 4 ambazo ni D mbili ama C na E.
“Ninatoa rai kwa wazazi na walezi wa vijana wenye sifa hizo kuweza kufika kwenye maonesho haya kwa minajili ya kupata utaratibu utakao wawezesha kujiunga na chuo hicho,” amesema Dkt.Panga.
Aidha Dkt.Panga ameeleza kwamba mbali na utoaji wa elimu chuo kikuu hicho huwawezesha wanafunzi kukabiliana na changamoto za ajira kwa kuwatafutia nafasi za kazi pindi wanapohitimu masomo yao.
Amesema chuo kikuu cha ushirikiana moshi kinwaazingatia watu wenye mahitaji maalumu kwa kuwapa nafasi za kuendelea na masomo hayo katika ngazi mbalimbali.
Dkt.Panga amewataka wazazi na walezi kutembelea banda la chuo cha ushirika moshi ili kupata maelekezo ya namna ya kujiunga na masomo.
Maonesho hayo yameanza julai 26 mwaka huu ambapo mgeni rasmi anatarajia kuwa waziri wa elimu sayansi na teknolojia Profesa Joyce Ndalichako ambayo yamebeba kauli mbiu isemayo ‘kuendelea kukuza na kudumisha uchumi wa kati kupitia elimu ya juu, sayansi na teknolojia.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito