December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kiungo mpya wa Yanga Carlinhos,

Wema Sepetu amkaribisha Carlinhos kwa mikono miwili Yanga

Na Mwandishi Wetu, Times Majira Online

MALKIA wa filamu hapa nchini anayetamba na Tamthilia yake mpya ‘Karma’, amemkaribisha kiungo mpya wa Yanga Carlinhos kwa mikono miwili ili aweze kuipa mataji timu yao msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Carlinhos, mwenye umri wa miaka 25 raia wa Angola, ni miongoni mwa wachezaji wapya wa Yanga waliosajiliwa msimu huu, huku akitua katika ardhi ya Tanzania na kupata mapokezi makubwa jambo linalomfanya kuwa na deni kubwa katika klabu hiyo.

Akiweka wazi hilo kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram Wema amesema, wao wanchotaka ni mataji ndio waweze kuongea Lugha nyingine.

“Tunachotaka sisi mpate Ubingwa tena mara saba alafu ndio tuanze kuongea lugha moja. Na zitabaki saba hivyo hivyo maana Ubingwa ni wetu roundi hii. Karibu sana Carlinhos,” ameandika Weama.