December 26, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wema awajibu wanaomsema kuhusu matangazo ya waganga

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MALKIA wa filamu hapa nchini Wema Sepetu, amewajibu wale wote wanaomsema kuhusu matangazo ya waganga yanayoonekana kwenye Ukurasa wake wa Instagram na kuwataka wasimfuatilie.

Akizungumzia hilo usiku wa kuamkia leo katika Birthday ya msanii wa muziki wa Bongo fleva mwenye vituko vingi hapa nchini GigyMoney, Wema amesema anashangaa sana kuona watu wakimduatilia wakati yeye huwa hamfuatilii mtu.

“Jamani nashangaa kuona watu wakinifuatilia kila ninalolifanya, mbona mimi huwa simfuatilii mtu, naomba mniache kila mtu ana mambo yake ya kufanya,” amesema Wema.