January 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

WAZIRI Ummy:Punguzeni kula sukari,chumvi na mafuta

Na Mwandishi Wetu.

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kujilinda na magonjwa yasiyo ya kuambukiza kwa kufuata miongozo ya watalaam ikiwemo kupunguza vitu kama chumvi, mafuta na sukari katika vyakula.

Waziri Ummy Mwalimu ameyasema hayo katika mdahalo wa Space katika mitandao wa Kijamii ulioandaliwa na kampuni ya Mwananchi juu ya miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ikulu.

“Changamoto kubwa kwa sasa hivi ni ongezeko ya magonjwa yasiyo kuambiza kama saratani, moyo na mengine, pia magonjwa ya figo, na ni gharama kubwa sana kuyatibu,”amesema na kuongeza”

Punguzeni chumvi, sukati na mafuta ilikujilinda na magonjwa hayo yasiyo ya kuambukiza, ili nimewekea mkazo sana ilituende kulimaliza,lakini

pia
tunaenda kuimarisha Afya ya Jamii mfano Afya ya Akili, magonjwa yasiyo ya kuambukiza, uzazi na mengine,” amesema Waziri
Mwalimu.