Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uswisi nchini Tanzania Mhe.Didier Chassot kwenye ukumbi wa Wizara jijini Dodoma.
Katika mazungumzo yao Waziri Ummy ameishukuru Serikali ya Uswisi kwa kuendelea kuchangia mfuko wa afya wa pamoja (Health Sector Basket Fund) ambao unalenga kuimarisha huduma za afya ya msingi nchini.
Aidha, Mhe Ummy ameishukuru Serikali ya Uswisi kwa kushirikiana na Serikali katika jitihada za kutokomeza ugonjwa wa Malaria kupitia Taasisi ya Swiss TPH.
Naye, Balozi Chasott ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kuhakikisha wananchi wanafikiwa na huduma za afya. Amesema kuwa nchi yake itaendelea kuipa kipaumbele sekta ya afya katika msaada inayoipatia Tanzania.
More Stories
Rehema Simfukwe atoboa siri sababu kuimba wimbo wa Chanzo
Tanzania ipo tayari kupokea wakuu wa nchi,mkutano wa nishati-Dkt.Kazungu
Chunya yafikiwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano