Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amekutana na kufanya mazungumzo na wamiliki wa kampuni za mafuta nchini pamoja na viongozi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati zinazoshughulikia Sekta ndogo ya mafuta na gesi.
Kikao hicho kimefanyika leo Machi 04, 2026 katika Ofisi Ndogo za Wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.

Ndejembi amewahakikishia wadau hao uhakika wa upatikanaji wa mafuta nchini na kuwasisitiza kuzingatia sheria na kanuni za ufanyaji wa biashara ya mafuta nchini.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamishna wa Mafuta kutoka Wizara ya Nishati, Bw. Goodluck Shirima, Mkurugenzi Mtendaji wa EWURA Dkt. James Mwainyekule, Mtendaji Mkuu wa TPDC ,Mussa Makame, Kaimu Mtendaji Mkuu wa PBPA Bruno Tarimo,Mwakilishi wa TRA pamoja na wamiliki wa Kampuni za Mafuta.


More Stories
Mhitimu asiyeona aeleza mafanikio ya useremala VETA
JNHPP: Ndoto ya Nyerere yatimia,Rais Samia apongezwa
Rais Samia aagiza wakuu wa Mikoa kujiandaa na udhibiti wa Athari za El Nino