December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Waziri Ndalichako atembelea Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi

Na Mwandishi Wetu TimesMajira Online, Morogoro

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako ametembelea Mradi wa Ujenzi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi (Mbigiri) Mkoani Morogoro kujionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.

Akizungumza katika ziara hiyo, Waziri Ndalichako amewataka watendaji wa mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho pamoja na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhakikisha wanasimamia ujenzi wa mradi huo ili uweze kukamilika wa wakati.

“Niwaombe sana watendaji wa mradi huu wa ujenzi wa kiwanda pamoja na uongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kuhakikisha mna msimamia kwa karibu mkadarasi anayetekeza ujenzi wa mradi huu ili aweze kukamilisha jukumu hili kwa muda uliopangwa,” alisema Waziri Ndalichako

“Nimezunguka katika maeneo mbalimbali ya ujenzi wa mradi huu, hivyo niwasihi kuongeza watendaji ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda kwa haraka,” alisema

Aliongeza kuwa, kukamilika kwa kiwanda hicho kutaleta manufaa kwa Taifa ikiwemo kusaidia kuongeza kwa uzalishaji wa sukari nchini sambamba na kutoa fursa za ajira kwa wananchi ambao watakuwa wakifanya kazi katika kiwanda hicho.

Kwa Upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Prof. Jamal Katundu alisema kuwa maelekezo yote yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri yatatekelezwa ili kukamilisha ujenzi wa mradi huo.

Naye Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Bw. Masha Mshomba aliahidi kufanyia kazi maelekezo yaliyotolewa na Mheshimiwa Waziri Ndalichako na kumhakikishia kuwa watashirikiana na Mkandarasi katika kufanikisha ujenzi wa mradi huo.

Ziara hiyo ya Waziri Ndalichako ililenga kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi Mradi wa Kiwanda cha Sukari ca Mkulazi pamja na kukagua mashamba ya Miwa ya kiwanda hicho ili kujionea hatua za iliyofikiwa kuelekea kwenye uzalishaji wa sukari na muekekeo wa uchumi wa viwanda nchini.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako akitazama maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Baadhi ya watendaji wa kiwanda cha Sukari cha Mkulazi wakisikiliza maelekezo ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Mkandarasi wa Kiwanda Mradi huo Mhandisi Jastine Mosha (kushoto) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako akiwa ameongozana na watendaji wa kiwanda hicho alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof. Joyce Ndalichako (wa nne kutoka kushoto) akisistiza jambo kwa watendaji wa kiwanda hicho alipofanya ziara ya kukagua na kujionea maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kiwanda hicho kilichopo Mkoani Morogoro.