March 21, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Pinda aipongeza VETA kwa hatua iliyopiga miaka 30

Na Penina Malundo,Timesmajira

WAZIRI Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda ameipongeza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA)kwa hatua kubwa waliyoipiga katika mafunzo ya ufundi stadi na Ubunifu kwa vijana.

Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipotembelea Kongamano la maadhimisho ya miaka 30 ya VETA,lililofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam,amesema VETA ikiendelea na kujiboresha zaidi kiteknolojia itaweza kufika mbali na kuwa mkombozi kwa vijana wengi.

Amesema Ufundi Stadi,Mafunzo na Ubunifu na mambo ambayo katika maisha ya mwanadamu hayawezi kukwepeka kwani yanakuwa ni sehemu ya maisha ya mtu na ya maendeleo ya taifa.

”Nawapongeza sana viongozi wa VETA na mnastahili kupewa pongezi kwa kazi kubwa mliyoifanya hadi sasa.Nimeambiwa kwamba kwa sasa kuna vyuo vya ufundi na mambo mengine yanayohusiana na ubunifu takribani 80.

”Na vyuo hivyo vipo wilaya kwa wilaya na sehemu nyingine vipo  wilaya na mkoa na vyote vinaangaika na eneo la kutoa maarifa kwa vijana ili waweze kutambua kwamba wanaishi katika ulimwengu unaozungukwa na fursa,”amesema.

Aidha amesema vitu vyote vinavyofanywa na kufundishwa na VETA ni vitu ambavyo mwanadamu anavihitaji.”Nndani ya mafunzo wanayoyatoa kuna kilimo,ufugaji,uvuvi hivyo ukitazama huduma za jamii hawa mafundi stadi ndio nafasi zao na wao kuomba ajira katika kupata kazi,”amesema

Pinda amesema amefarijika kuona Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC)kikiwa na mahusiano mazuri na VETA,hii inamaana wawekezaji wanapokuja nchini kuwekeza wanatumia vijana wa VETA katika kufanya shughuli zao.

”Nimefurahi sana linki hii itasaidia kuwapeleka vijana katika maeneo stahiki na ni muhimu kuweka mahusiano na taasisi nyingine,katika kuwaunganisha na  VETA katika kuwasaidia vijana katika,”amesema.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa VETA,CPA.Anthony Kasore amemshukuru Waziri Mstaafu Pinda kufika katika kongamano hilo na kutembelea mabanda mbalimbali.

”Si kwamba Waziri Pinda ni mgeni VETA bali amefika kwenye kongamano hili kujionea VETA ilipofikia maana akiwa Waziri Mkuu alihusika kusimamia maboresho makubwa yaliyofikiwa na VETA,”amesema.

Amesema Waziri Pinda ameondoa shaka na kuamini gurudumu hili la mafunzo stadi yanakwenda vizuri,kwani bado amekuwa mtu wa kuwashauri waendaje.